Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 28Article 560161

Tabloid News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TETESI: Diamond Amnunulia Ndinga Kali Mrembo Wake wa Rwanda?

Diamond na Ms Ris Eddy. Diamond na Ms Ris Eddy.

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambae baada ya ukimya wa muda mrefu kwa sasa inadaiwa kwamba, yupo katika mahusiano ya kimapenzi na mrembo mwenye asili ya Rwanda na Tanzania anayefahamika kwa jina la Ms Ris Eddy amemnunulia gari jipya la kifahari.

Huku taarifa zikieleza kwamba kwa sasa wawili hao wapo Visiwani Zanzibar wakiponda raha katika hotel moja ya kifahari Visiwani humo.

Ifahamike kuwa mwanadada Ris Eddy ni rafiki wa kutupwa wa Wema Sepetu ambae pia amewahi kuwa kwenye mahusiano na Diamond.

Kupitia mitandao ya kijamii zipo picha inamuonyesha mwanadada Ris Eddy akiwa katika gari jipya, huku akishukuru kwa zawadi na kuweka emoji ya Simba na alimasi. Baada ya hapo ndipo imedhithibitisha kwamba yupo kwenye penzi na Diamond.

Juma Lokole ameweka picha katika ukura wake wa Instagram ambayo inamuonyesha mrembo huyo akiwa katika gari jipya na kuandika kwamba kwamba, kampa gari? Jambo ambalo limechukuliwa kama ni ujumbe tosha wa uwepo wa penzi hilo.