Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 09 18Article 558238

Tabloid News of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TETESI: Huyu ndiye mpenzi mpya wa Harmonize

Harmonize na Yolo. Harmonize na Yolo.

UNAAMBIWA staa wa Bongo Flava, Rajabu Abdul a.k.a Harmonize ameripotiwa kuwa kwenye mahusiano mapya na mrembo anayetajwa kwa jina maarufu la Yolo The Queen.

Tetesi za Harmonize kuwa kwenye penzi jipya zilianza kuvujishwa na mitandao ya nchini Burundi kisha Rwanda na baadaye Uganda, baada ya star huyo kudaiwa kuwa ndiye pekee mwenye uwezo wa kuweka maoni kwenye ukurasa wa Instagram wa Yolo.

Mrembo huyo aliposti picha kali na kuandika; “Am an example to follow…” Baada ya hapo ndipo mtu mzima Konde Boy ‘aka-like’ picha na ujumbe huyo kabla ya mrembo huyo kuibuka na ‘kum-tag’ Harmonize huku akifunga sehemu ya maoni kwa mtu yeyote isipokuwa Harmonize pekee.

Hata hivyo, baada ya jambo hilo kutokea, Harmonize ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya kimuziki nchini Marekani, naye akaachia ujumbe ambao unaashiria kwamba, kwa sasa hayupo tena singo.

Katika majibizano na DJ wake, DJ Seven, Harmonize ameandika; “Ningekuwa single enzi zangu unge-enjoy jana… Ukubwa huu miye wa kulala saa 4 nabembeleza…”

Lakini kwa muonekano wa picha tu, mrembo huyo ambaye amekuwa akipambanishwa na aliyekuwa mpenzi wa Harmonize, Kajala Masanja anaonekana ni pisi kali ambaye endapo itathibitika ni wapenzi, basi wataisimamisha Afrika Mashariki.

Katikati ya gumzo hilo, Gazeti la IJUMAA bila kuthibitisha kama kweli ni wapenzi, limetafuta kupitia chanzo usichokijua kuhusu mrembo huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Yolo The Queen ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) wa Burundi mwenye maskani yake nchini Uganda.

Yolo mwenye umri wa kati ya miaka 22 na 25, anatajwa kuwa ni modo na balozi wa kutangaza mavazi huku mambo mengine akiyaweka kuwa ni binafsi.

Kuhusu kuolewa, Yolo anatajwa kuwa yupo singo na katika utambulisho wake kwenye mitandao anasema yupo singo na hana haraka ya kuwa kwenye mapenzi.

Pia anatajwa kwamba ni mwandishi wa habari kwa kiwango cha Diploma, lakini hajawahi kuifanyia kazi fani yake yake hiyo hivyo mashabiki wengi wa Konde Boy wanasikilizia kama jamaa huyo atamtambulisha rasmi.

Kabla ya hapo, Harmonize alikuwa kwenye penzi na Kajala baada ya ndoa yake na Sarah Michelloti kuvunjika akiwa pia amepita kwenye mikono ya mwigizaji Jacqueline Wolper au Mama P kwa sasa.