Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 11Article 562642

Burudani of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Takwimu za Zuchu Youtube ni balaa

Mwimbaji Zuchu Mwimbaji Zuchu

TANGU Januari hadi Septemba kwa mwaka 2021, namba za Zuchu kutoka Lebo ya WCB zinatisha.

Zuchu amekuwa ndiye msanii wa kike anayeongoza kutazamwa zaidi kwenye Mtandao wa YouTube kwa upande wa nchini Tanzania.

Kwa kipindi chote, Zuchu amekuwa akipata views (watazamaji) zaidi ya milioni 10 kila mwezi ambapo Februari ndipo alipata views nyingi zaidi ikiwa ni zaidi ya milioni 25.

Zuchu ambaye alisainiwa WCB Aprili, 2020, mwaka huu ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike Tanzania kufikisha views zaidi ya milioni 100 kwenye YouTube.

Utakumbuka Januari mwaka huu, Zuchu aliachia wimbo wake wa Sukari ambao video yake imefikisha views zaidi ya milioni 50 na ndiyo video pekee iliyotoka mwaka huu Tanzania na Afrika Mashariki yenye views nyingi zaidi kunako YouTube.