Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 13Article 571048

Filamu of Saturday, 13 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

The Rock Afunguka Sababu Ya Kukojoa Kwenye Chupa

The Rock The Rock

Dwayne Johnson (49) almaarufu @therock staa wa filamu za mapigano kutoka Marekani, aliyeigiza filamu kama; Jumanji, Jungle Cruise, Moana, Skyscraper, Rampage na zingine kibao, ameweka wazi sababu inayomfanya akojoe kwenye chupa wakati wa mazoezi akiwa ‘gym’ kuwa ni kukosekana kwa bafu katika maeneo anayofanyia mazoezi.


Tetesi za ‘The Rock’ kukojoa kwenye chupa wakati wa mazoezi zilianza kusambaa tangu mwaka 2017 kupitia mtandao wa Instagram ambapo yeye mwenyewe alikiri kuwa anafanya kitendo hicho huku akiwa hajaweka wazi sababu ya kufanya hivyo.


Baada ya miaka minne kupita, ‘The Rock’ ameweka wazi sababu inayomfanya akojoe kwenye chupa wakati wa mazoezi akiwa ‘gym’, kuwa sehemu anazofanyia mazoezi hazina bafu na ndiyo maana inamlazimu kukojoa kwenye chupa.


“Usually the gyms that I work out in don’t have a bathroom because they’re the iron paradise. They’re just hot, sweaty and dirty.” Alisema The Rock.
Mara ya mwisho kukojoa kwenye chupa ilikuwa lini?