Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 12 30Article 582001

Filamu of Thursday, 30 December 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

The Rock Aikataa Fast & Furious 10

The Rock Aikataa Fast & Furious 10 The Rock Aikataa Fast & Furious 10

Muigizaji Dwayne Johnson maarufu kama the “The Rock” amekataa ombi la kurejea kuigiza muendelezo wa filamu ya Fast & Furious sehemu ya 10.

The Rock katika interview yake na CNN iliyochapishwa siku ya jana amekataa ombi la Vin Diesel kurejea katika Fast & Farious na kumkosoa kwa kitendo chake cha kuongolea suala hilo katika mitandao ya kijamii kwa kuwahusisha watoto na marehemu Paul Walker.

“Nilishangazwa sana na post ile ya Vin Diesel, mwezi wa sita mwaka huu niliongea nae faragha na kumwambia sitaweza kuigiza tena filamu hiyo ila nitatoa ushirikiano wangu katika kuandaa filamu hiyo ili kuhakikisha inafanikiwa na hata washirki wengine wote niliongea nao na walinielewa,” Majibu ya The Rock.

Je unadhani Fast & Farious itatoboa bila The Rock?