Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 18Article 572353

Burudani of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

The Rock ataka kupewa nafasi ya kuwa 'James Bond'

The Rock ataka kupewa nafasi ya kuwa play videoThe Rock ataka kupewa nafasi ya kuwa "James Bond" kwenye filamu zake

Muigizaji Dwayne “The Rock” Johnson amefunguka kuwa anataka kuwa James Bond anayefuata.

Muigizaji huyo alifunguka kuhusu kupendezwa kwake na jukumu hilo kutokana na Daniel Craig kustaafu kutoka kwenye filamu za Bond baada ya "No Time To Die".

“Ndiyo, babu yangu alikuwa mhalifu wa Bond katika "You Only Live Twice" pamoja na Sean Connery. hivyo hiyo itakua jambo kubwa sana kama nikipewa hiyo nafasi,” - The Rock

“Ningependa kufuata nyayo zake na kuwa Bond anayefuata. Sitaki kuwa mhalifu. Lazima niwe Bond."