Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 08Article 562045

LifeStyle of Friday, 8 October 2021

Chanzo: Powe1051

Tiwa Savage asimulia alivyotumiwa video yake ya faragha

Tiwa Savage asimulia alvivyotumiwa video yake ya faragha Tiwa Savage asimulia alvivyotumiwa video yake ya faragha

Mwanamuziki Tiwa Savage kutoka Nigeria kwenye mahojiano yake leo na kituo cha Power 105.1, nchini Marekani, akizungumza kwenye show ya 'The Angie Martinez Show' amefunguka kuwa jana ametumiwa video yake akiwa FARAGHA (mkanda wa ngono) na mpenzi wake.

Tiwa ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake binafsi, amekiri kwamba, video hiyo inaonyesha kuwa ni yake kwani anaonekana akiwa na mpenzi wake aliyenaye sasa.

"Jana wakati nikiwa njiani ndani ya gari langu, meneja wangu alinitumia ujumbe kwa njia ya sms kwamba kuna video amenitumia niitazame. Nilishtuka nilipoitazama na kujiuliza kuwa ameitoa wapi, ilikuwa kama dakika 20 kufanyika kwa tukio hilo" Tiwa Savage

"Meneja alinieleza video hiyo ya FARAGHA alitumiwa na kijana tuliyenaye kwenye timu yetu" - aliendelea Tiwa Savage, "Nilichanganyikiwa na kumuuliza meneja wangu kuwa tunafanyaje?

"Meneja akaniuliza ni kiasi gani anahitahiji tumpatie? Nikamjibu hapana, kwa sababu tukimpa pesa leo, atarudi tena baada ya miezi 2 mbele atahitaji tena pesa, kwahiyo siwezi ruhusu mtu kuniibia kwa kitu ambacho sio halali"