Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 12Article 551251

Burudani of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tozo ya Mirabaha kuwa rafiki – Cosota

Tozo ya Mirabaha kuwa rafiki – Cosota Tozo ya Mirabaha kuwa rafiki – Cosota

Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) kimeweka wazi kuwa tozo za mirabaha kwa rasimu ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2021 itakuwa rafiki.

Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2021 na Mwanasheria wa Cosota Lupakisyo Mwambinga katika kikao cha kukusanya maoni ya rasimu ya kanuni ya leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma kilicholenga kupata maoni ya tozo za mirabaha zilizopangwa kwa matumizi ya Muziki katika vyombo vya habari.

Alisema maoni yote yanayotolewa na wadau yatafanyiwa kazi kwani lengo ni kujenga mazingira rafiki ya tozo za mirabaha ili ziweze kulipika.

“Maoni yote tumeyapokea na tutayafikisha panapohusika na kwa wadau wa kebo tumepokea maoni yenu na changamoto zenu tutaziwasilisha ofisini ili zifanyiwe kazi na naomba mfahamu ya kuwa kikao hichi kimelenga kujenga mazingira rafiki ya tozo hii ya mirabaha iweze kulipika,” alisisitiza