Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 12Article 570565

Filamu of Friday, 12 November 2021

Chanzo: Habarileo

Tuzo za Oscar kufanyika nchini

Tuzo za Oscar kufanyika nchini Tuzo za Oscar kufanyika nchini

TUZO za kimataifa za filamu za Oscar (WFF) zinatarajiwa kufanyika nchini mwaka 2023 baada ya serikali kukubaliana na mwasisi wa tuzo hizo, Dk Fasi Khuramm.

Tuzo hizo zinazokusanya mastaa kutoka nchi mbalimbali duniani mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Dubai Novemba 20, zikishirikisha jumla ya wasanii 150 wanaogombea nafasi tofauti kutafuta washindi 50.

Wiki hii serikali ilikuwa na ugeni wa Dk Khuramm na wajumbe wengine akiwepo mwigi- zaji kutoka India, Sanjay Dutt wakizungumzia namna ya kuinua sekta ya filamu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Filamu Tanzania, baada ya mazungumzo yaliyowahusisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Dk Kiagho Kilonzo na wasanii mbalimbali, Dk Khuramm alitangaza ujiowa tuzo hizo nchini. “Dk Khuramm aliwaeleza wadau umuhimu wa tuzo hizo na kutangaza kuwa zitafanyika hapa nchini mwaka 2023,” alisema Dk Kilonzo.

Kwa upande wake Bashungwa alisema wamejadiliana na Sanjay Dutt kuleta wataalamu kutoka Bollywood, watakaoshirikiana na Bodi ya Filamu pamoja na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kufundisha namna bora zaidi ya utayarishaji wa kazi za filamu.

“Tumejadili kuhusu utayarishaji wa filamu, kuna fursa ya watayarish- aji wa filamu kutoka India na Tanzania kushirikiana kutayarisha filamu ya pamoja kwa kutumia mandhari za nchi zote mbili ili kutangaza vivu- tio vya utalii,” alisema.

Bashungwa alisema ujio wa msanii huyo nguli utasaidia kuendeleza safari ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour.

Alisema Tanzania inatekeleza mkakati wa kubainisha na kutangaza maeneo mazuri ya kupiga picha za filamu hapa nchini kwani baadhi yamevutia kampuni mbalimbali kutoka nje ya nchi kutayarisha filamu zao zikiwemo Amazing Race, Criminal Mind, Serengeti, Forces of Nature, the Mating Game, On the Steps of Kuwait Sailor, Tanzania Beyond the Wild, Extreme Treks, Pechino Express, Big Cat, Ben Fogless, the Great African Migration na Night of the Lotus.