Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 12Article 585271

Burudani of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Unaambiwa Tanasha na Omah Lay ni Kitu na Boski

Unaambiwa Tanasha na Omah Lay ni Kitu na Boski Unaambiwa Tanasha na Omah Lay ni Kitu na Boski

PAMOJA na kukanusha mara kadhaa kwamba hawavunji amri ya sita, lakini madai yanazidi kushika kasi kwamba, baby mama wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna na msanii wa Nigeria, Omah Lay ni kitu na boksi.

Hii ni baada ya wiki iliyipita kunaswa kwa mara nyingine wakiponda raha huko Pwani ya Malindi nchini Kenya.

Katika mahojiano yake miezi kadhaa iliyopita, Omah Lay alikiri kuwa na mpenzi nchini Kenya huku akigoma kumtaja.

Kumekuwa na uvumi kuwa mwanamuziki huyo amejaza nafasi iliyoachwa na Diamond zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya video iliyoonesha wakijiburudisha pamoja kuenezwa mitandaoni katikati ya mwaka uliopita.