Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 03Article 540814

Burudani ya

Chanzo: eatv.tv

Usilojua kuhusu 'Ukisikia Paah' ya JCB

Usilojua kuhusu 'Ukisikia Paah' ya JCB Usilojua kuhusu 'Ukisikia Paah' ya JCB

Ni miaka 10 hivi imepita tangu Rapper JCB kutoka Watengwa alipoachia wimbo wake ‘Ukisikia Paah!!’ aliowashirikisha Fid Q, Jay Moe na Chidi Beenz na kupata mafanikio makubwa ikiwemo Tuzo 2 za KTMA mwaka 2011.

Submitted by Telesphory on Alhamisi , 3rd Jun , 2021 Msanii JCB

Remix ya wimbo huo wa The Arusha Legend Hip Hop Emcee JCB ndio wimbo wa kwanza kurekodiwa ndani ya studio za Tongwe Records chini ya watayarishaji J Murder na J Rider, huku ukitengeneza rekodi kwa JCB kuondoka na Tuzo ya Best Hip Hop Song na Best Collaboration Song mwaka 2011.

Mwezi Oktoba 9, 2014 kupitia instagram JCB aliandika “Ngoja tutupe nyuma kidogo, ilikuwa 2011 pale nilipo ibuka na Tuzo mbili za HIP HOP kwa kweli ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa wana wote, pande zote kitaa na kila pembe..UKISIKIA paah......vuuuuuuuuuuh Tongwa recods bebiiiii”

Join our Newsletter