Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 23Article 553042

Burudani of Monday, 23 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

WHOZU Akiri Kukamatika Kwa Tunda

Msanii wa Bongo Fleva Whozu akiwa na Mpenzi wake Tunda. Msanii wa Bongo Fleva Whozu akiwa na Mpenzi wake Tunda.

Msanii wa Bongo Fleva, Oscar Lelo au Whozu anafunguka kuwa, amekamatika ile mbaya baada ya hisia zake kimapenzi kutekwa na baby mama wake, Tunda .

Whozu anasema kuwa, upendo alionao kwa mpenzi wake huyo hauwezi kuelezeka kwani kuna muda anatamani aitie vyombo vya habari na maeksi wake wote awaambie ni jinsi gani alivyo na furaha kwa sasa.

“Nashindwa sijui hata niongee kitu gani ila Tunda ananifanya nainjoi sana. Huo ndiyo ukweli usiopingika kwamba nimekamatika kwa Mama Lola, huyu mwanamke ananipa ninachotaka,” anasema Whozu ambaye miezi michache iliyopita alifanikiwa kupata mtoto wa kike na Tunda.