Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 07 30Article 548509

Mitindo/Urembo of Friday, 30 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Warembo 10 kuchuana Miss Morogoro leo

Warembo 10 kuchuana Miss Morogoro leo Warembo 10 kuchuana Miss Morogoro leo

WAREMBO 10 leo wanatarajia kuwania taji la kumsaka Miss Morogoro 2021, ambapo kila mmoja atamba kushinda na kushiriki Miss Kanda Mashariki.

Mratibu wa shindano hilo, Alexander Nikitas alisema jana mjini hapa kuwa maandalizi yote yamekamilika na hatua zote za tahadhari kujikinga na ugonjwa wa Corona zimezingatiwa.

“Siku ya fainali ambayo ni Julai 30 (leo) inayofanyika ukumbi wa hoteli ya Oasis ya mjini hapa, tumeruhusu idadi ndogo ya watu na kila mmoja anatakiwa kuvaa barakoa, na unawaji wa mikono kwa maji tiririka kabla na baada ya kutoka kwenye ukumbi,” alisema Nikitas.

Mratibu huyo aliwataja warembo wanaoshiriki shindano ni Theresia Yasini (23), Emanuela Silayo (20), Easter Bulembwa (23), Halima Wangare (20), Yuster Benjamin (20), Neema George (20), Raudhat Khamis (20), Proscovi Mitto (22) na Chipengwa Julius (20).

Naye aliyekua Miss Morogoro wa kwanza mwaka 1995, Rona Lyimo aliwataka warembo hao kutumia nafasi zao kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Morogoro,zikiwemo za utalii na za nchi kwa ujumla na si kutumia nafasi zao katika matendo yasiyoipandeza jamii.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Morogoro, Norah Mzeru, Katibu wa Mbunge huyo, Ismail Kifaru aliwasihi warembo wanaoshiriki shindano hilo kubuni fursa za kiuchumi kwani zitawaingizia kipato na kuwa mfano bora katika jamiii.

Kifaru alisema, jamii kwa sasa inahitaji elimu zaidi kuhusu masuala ya ujasiriamali na hivyo kwa upande wao wanatakiwa wawe kioo cha jamii.