Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 08 25Article 553723

Mitindo/Urembo of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Warembo 20 kuchuana kuwania Miss Tanzania Kanda ya Mashariki

Warembo 20 kuchuana kuwania Miss Tanzania Kanda ya Mashariki Warembo 20 kuchuana kuwania Miss Tanzania Kanda ya Mashariki

Morogoro. Shindano la kumsaka mlimbwende (Miss Tanzania 2021) Kanda ya Mashariki linatarajia kufanyika mkoani Morogoro kwa kushirikisha warembo 20 kutoka mikoa minne inayoundwa kanda hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa kampuni ya Tips Forum, Mhandisi Nancy Matta amesema fainali ya mashindano hayo yatafanyika Septemba 24 Morogoro kwa mikoa shiriki ikitoa warembe watano katika kuwania taji hilo.

Mhandisi Nancy ametaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Lindi, Pwani, Mtwara na Morogoro wenyeji ambao tayari shindano la Miss Tanzania mkoa huo limefanyika kwa kupata wawakilishi wa shindano la Miss Tanzania 2021 Kanda ya Mashariki.

“Kabla ya shindano la Miss Tanzania kanda ya Mashariki, warembo watashiriki mashindano mengine ya likiwemo la Miss vipaji (Talent), Top Model amesema Mhandisi Nancy.

Mhandisi Nancy ambaye ni Miss Mbeya 2018/2019 amesema kuwa lengo la kufanya mashindano hayo kurudisha heshima Miss Tanzania kanda ya Mashariki.

“Kampuni ya Tip Forus ndio imeandaa mashindano ya Miss Tanzania 2021 kanda ya Mashariki katika kuelekea kuwapata washindi ambao wataingia kwenye shindano la Miss Tanzania 2021 ambapo huko tutapata wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya mrembo wa dunia hapo baadaye.”amesema Mhandisi Nancy.

Mratibu wa shindano la Miss Tanzania 2021 kanda ya mashariki, Twiza Mbaruku amesema wana hamu ya kurejesha mvuto mashindano hayo kwa sababu yalipoteza mvuto.

“Tunalengo kubwa ya kurejesha amani hasa kwa kufanya matendo mazuri na jamii, wadau na Serikali ambapo wamepoteza amani katika mashindano haya kwa kuwasapoti mabinti wao na tuna hamu katika sekta ya sanaa ya urembo.”alisema Twiza.

Meneja wa Samaki Sport Morogoro, Godfrey Mlingwa amesema wamejindaa kukaribisha wadau wa sekta ya sanaa ya urembo kupitia Miss Talent ambayo itafanyika Septemba 22 mwaka huu Samaki Sport.

Shindano la miss Tanzania kanda ya mashariki, warembo wake wanatarajia kuweka kambi katika mikoa miwili ya Pwani kisha kufuatiwa na Morogoro ambapo litafanyika shindano lenyewe la kumpata ushindi wa Miss Tanzania 2021 kanda ya mashariki ili kupata washindi watakaowakilisha shindano la miss Tanzania taifa mwaka huu.