Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 12 18Article 579445

Mitindo/Urembo of Saturday, 18 December 2021

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Watoto 30 kutawala jukwaa onyesho la mitindo kesho

Watoto 30 kutawala jukwaa onyesho la mitindo kesho Watoto 30 kutawala jukwaa onyesho la mitindo kesho

Jumla ya watoto 30 wanamitindo, wanatarajia kushiriki onyesho la Pendeza Kids Fashion Extravaganza 2021 linalofanyika kesho jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa tamasha hilo, Hadija Mwanamboka amesema juzi kuwa, lengo la onyesho hilo ni kuwashirikisha watoto kutoka kwenye mazingira na sehemu tofauti katika tasnia ya ubunifu mitindo.

Katika onyesho hilo, watoto watapita jukwaani wakiwa wamevaa mavazi yaliyobuniwa na wanamitindo Fiderine Iranga na Victoria Martin ambao wataonyesha umahiri wao katika ubunifu wa nguo za watoto. 

"Lakini tunaamini, onyesho litawasaidia kuboresha afya ya akili kwa watoto wanaolelewa kwenye vituo vya watoto yatima, litawawezesha watoto wenye ulemavu na hata kuwapa watoto waishio kwenye mazingira magumu jukwaa la kuonyesha uwezo wao kwenye sanaa na mitindo," amesema Mwanamboka.

Pia, amesema watoto wanamitindo wanaoshiriki ni 30 wakiwamo watoto wenye ulemavu kutoka Chama cha Watu wenye ulemavu Tanzania wilayani  Kinondoni

"Onyesho hili litafanyika kwenye Hoteli ya Hyatt kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa mbili usiku, mgeni rasmi atakuwa mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa," amesema.

“Hakutakuwa na kiingilio, ingawa kuna mialiko maalumu ya washiriki na watoto yatima pia wamealikwa kutoka vituo vya Mwandaliwa Orphanage na Ashura Foundation.”

Amesema baadhi ya waalikwa ni  Rita Paulsen , wabunifu mavazi na wanamitindo.