Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 06 07Article 541345

Burudani of Monday, 7 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wema Ataja Sababu Nyota Yake Kung’ara

Wema Ataja Sababu Nyota Yake Kung’ara Wema Ataja Sababu Nyota Yake Kung’ara

Wema Ataja Sababu Nyota Yake Kung’ara June 7, 2021 by Global PublishersKWA mara ya kwanza, mlimbwende wa Tanzania kwa mwaka 2006/07 ambaye ni supastaa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ametaja sababu iliyosababisha nyota yake kung’ara na isishuke hadi leo kuwa ni kujitambua na kujua ni nini anafanya.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake Bongo anasema kuwa, kabla ya yote anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake aliyompa hadi leo kwa sabbau ana kitu ndani yake ambacho wengine hawana, lakini pia kujitambua na kujua yeye ni nani ndiko kunamfanya aendelee kuwa juu kila siku.

“Mbali na kumshukuru Mungu kwa afya na uzima anaoendelea kunipa kila siku, lakini pia juhudi na nidhamu naamini ndivyo vitu vinavyonifanya nisishuke kirahisi, ingawa napigwa sana vita, lakini siku zote alichokipanga Mungu kamwe mwanadamu hawezi kukipangua,” anasema Wema.

Ni zaidi ya miaka kumi na tano sasa tangu mwanadada Wema awe Miss Tanzania, licha ya changamoto nyingi anazozipitia katika maisha, lakini hiyo haijamfanya ashuke na ndiyo kwanza unaweza kusema nyota yake inakua kila siku.

Stori; Memorise Richard, Dar

Join our Newsletter