Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 25Article 574000

Burudani of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wema Awatolea Povu Wanaomsema Kuishi Mbagala

Wema Sepetu Wema Sepetu

MALKIA wa Bongo Movies, Wema Sepetu amewatolea uvivu watu ambao wanamsema kuwa anaishi Mbagala sehemu ambayo ni inadaiwa kuwa ni ya hadhi ya chini ikilinganishwa na ukubwa wa jina lake, umaarufu wake Bongo na nje ya nchi.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari, Wema amesema; "Tuseme ningekua naishi Mbagala kweli kwani watu ambao wanaishi Mbagala sio binadamu? au hawafai? au hawatakiwi? Kwa sababu Mbagala pia ni sehemu kama sehemu zingine.

"Wanaoishi Mbagala sio wanyama wala wadudu ni watu kama watu wengine na mimi nimesema nilikua nikiishi kule kwa sababu ya karma, kazi ndio ilinifanya niishi kule nimemaliza sina tena kitu kinacho nifanya niishi kule...." amesema Madam Wema.