Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 23Article 573619

Burudani of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wema: Mkiniona na Mwanaume Mjue ni Mme Wangu

Wema Sepetu Wema Sepetu

REMBO mwenye jina kubwa kunako Bongo Movies, Wema Sepetu @wemasepetu amefunguka sababu ya yeye kuficha uhusiano wake wa kimapenzi.

Wema anasema kuwa, hayupo tayari kumuani mpenzi wake kwa wakati wote alipofanya hivyo; yaani kuwaanika wapenzi wake, hakuna chochote alichokipata.

Anasema kuwa, kama kuna siku watu watamuona na mpenzi wake, basi huyo atakuwa ndiye mumewe, ila kwa sasa watu waendelee tu kudhani kwamba yupo singo au yupo kwenye mapenzi.

“Sidhani kama nipo tayari kufanya hivyo, sipo tayari kumuanika mpenzi wangu kwa sasa, angalau tukiwa kwenye ndoa, lakini siku mtaniona na mtu mjue ni mume wangu,
lakini kwa sasa tuendelee tu kudhani nipo kwe uhusiano au la hivyo tu...” Anasema