Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 10 13Article 562936

Burudani of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wema Sepetu: "Natamani Kupendwa"

Wema Sepetu: Wema Sepetu: "Natamani Kupendwa"

Muigizaji mrembo wa filamu za Tanzania, Wema Sepetu amefichua kuwa kwa sasa hana mpenzi.

Uhusiano wa kukumbukwa wa Wema ulikuwa kati yake na muimbaji nyota Mtanzania Diamond Platnumz Muigizaji huyo wa filamu za Bongo, walikuwa wanapendana sana kabla ya wao kutengana mwaka 2014.

Wakati mpenzi wake wa zamani Diamond, akisonga mbele na maisha na kuingia katika uhusiano mpya, muigizaji huyo amethibitisha kuwa bado hajapata mchumba.

Mshindi huyo wa zamani wa Miss Tanzania, alikiri kuwa maisha yake kwa sasa hayajakamilika sababu ya kukosa mpenzi.

Sepetu alipakia video yake maridadi kwenye Instagram akidensi wimbo wa Tiwa Savage wa Somebody's Son.

Katika posti yake, alifichua kwamba ana matumaini kwamba atachumbiwa hivi karibuni.

"Mtoto wa mtu atanipenda sana siku moja.... nakwambia Mama wakwe, Mawifi, Mashemeji na Kadhalika mtaona wivu wa Ajab... (natania ytu mimi ni mtu mzuri) Sidhani kama mimi ni mgumu kupendeka... Au tuwaulize walopita..namisi kupendwa... lakini nina furaha...," alisema.

Diamond amuwaza Sepetu TUKO.co.ke iliripotia kuwa mama yake Diamond Platnumz, Mama Dangote, alidokeza kuwa mwanawe amekuwa akimuwaza mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu wakati aliachia wimbo wake mpya.

Hii ni baada ya nyota huyo wa Bongo kuachia wimbo mpya wa Naanzaje ambapo anamtaja mpenzi wake ambaye hawezi kumuwacha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliweka wazi hisia zake kwenye wimbo huo akisema unamkubusha mpenzi wake wa zamani ambaye alimpenda sana na walikuwa wakijifungia ndani ya nyumba kwa wiki moja.

Mama yake Diamond alipakia sehemu ya video ya wimbo huo kwenye Instagram akiia namna mwanawe amekuwa akitumia jina madam.

Kisha alimtaja Wema Sepetu akisema hayakuwa maneno yake mwenyewe bali ya mwanawe.

"Madam kama madam lakini sepewesewe aka sepenga @wemasepetu sio maneno yangu ni maneno ya Simba," aliandika.

Mama Dangote anaminika kuwa shabiki mkubwa wa Wema Sepetu, na anaonekana kuelewa ujumbe wa mwanawe ulikuwa unamlenga nani.