Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 11 22Article 573346

Burudani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wizkid aondoka na tuzo tatu AFRIMA 2021

Wizkid Wizkid

SUPASTAA wa Afropop, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kama Wizkid kutoka nchini Nigeria, usiku wa kuamkia leo Novemba 21, 2021, amefanikiwa kushinda tuzo tatu (3) za AFRIMA kwa mkupuo.

Wizkid alitajwa kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kiume, (Artiste of the Year), Wimbo Bora wa Mwaka (Song of the Year) Essence ft Tems, pamoja na Wimbo Bora wa Kushirikiana (Best Collaboration) Essence.

Wizkid amewabwaga wasanii wakubwa wakiwemo Burna Boy, Diamond Platnumz, Davido, Sarkodie na wengine.

Hafla ya utoaji wa tuzo za Afrima 2021, zimefanyika katika Hotel ya Eko, huko Lagos nchini Nigeria.