Uko hapa: NyumbaniBurudani2021 07 13Article 546859

Burudani of Tuesday, 13 July 2021

Chanzo: eatv.tv

Wizkid aweka historia Hot 100

Wizkid aweka historia Hot 100 Wizkid aweka historia Hot 100

Wimbo wa Wizkid Essence aliomshirikisha Tems umeweka historia mpya kwake, sasa ni rasmi umeingia kwenye chart kubwa za muziki ulimwenguni za Billboard Hot 100 na kushika namba 82 kwenye wiki yake ya kwanza.

Essence ni wimbo wa 4 kutoka kwenye album ya ''Made In Lagos'' na unakuwa wimbo wa kwanza toka nchini Nigeria kuingia kwenye chart za Billboard Hot 100 huku ikiwa ni  mara ya  3 kwa Big Wiz kuingia kwenye chart hizo na mara ya kwanza kwa Tems.Big Wiz aliwahi ingia kupitia "One Dance" ya Drake ambayo ilifanikiwa kushika namba 1 mwaka 2016 pia kupitia collabo yake na Beyonce "Brown Skin Girl" ambayo ilikaa namba 76 kupitia Billboard Hot 100.