Uko hapa: NyumbaniBurudani2022 01 14Article 585658

Burudani of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Za Ndaani Kabisa... Zuchu Akiolewa na Mondi Amekwisha!

Zuchu na Diamond Zuchu na Diamond

UKIACHANA na ishu ya kujiuzulu kwa Spika Job Ndugai, katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2021 kuingia 2022, miongoni mwa topiki ambazo ni za moto kwenye eneo la burudani ni ishu ya msanii Zuchu kuchumbiwa kwa siri na bosi wake pale WCB, Diamond Platnumz.

Pamoja na kwamba mama wa Zuchu, Bi Khadija amejitokeza hadharani kukanusha vikali ishu hiyo akidai Zuchu anamheshimu mno Diamond, lakini bado vyanzo vya ndani kabisa vimeendelea kuaminisha umma kwamba, Zuchu anaolewa na Diamond au Mondi.

Kwa mujibu wa Bi Khadija, uhusiano wa Diamond na Zuchu ni wa dada na ndugu huku akidai bosi huyo wa WCB huwa anamchukulia kama mama yake.

Bi Khadija anasema kuwa, baada ya kusikia jambo hilo, alimuita Zuchu na kukaa naye kitako kisha kumhoji kuhusu madai hayo na alimhakikishia kuwa Diamond amekuwa akionesha heshima kwake na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.

“Zuhura (Zuchu) aliniambia Diamond anamheshimu sana na hajawahi hata siku moja kumuambia vitu vya kipuzi. Nilishtuka maana watu walikuwa wanavumisha kupita kiasi.

“Nilishangaa mbona walivumisha kupita kiasi. Mimi mwenyewe sikushughulika sana. Nilimuuliza Zuhura mbona watu wanavumisha sana au kuna kitu chochote. Aliniambia hamna wala hajawahi kuvunjiwa heshima hata siku moja.

“Mimi nilichukulia kama kitu cha kawaida,” anasema Bi Khadija; gwiji wa muziki wa Taarab barani Afrika.

Hata hivyo, pamoja na maelezo ya Bi Khadija, lakini watu wa karibu wanasema hawawezi kupuuzia kabisa madai hayo kwani mara nyingi mastaa hao wameonekana kuwa na uhusiano usio wa kawaida wa ndugu au kaka na dada.

Wachambuzi mbalimbali wanasema kuwa, kama madai hayo ni ya kweli ni vyema Zuchu akafahamu vizuri hali ambayo anakwenda kukutana nayo hivyo achukue tahadhari kabla ya hatari.

Wadau hao wamejikita kwenye historia isiyo ya kusifiwa ya Diamond na wanawake ambao tayari amepita nao na wengine kuzaa nao.

Inaelezwa kwamba, Diamond anahukumiwa na listi ndefu ya wanawake.