Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 11 10Article 570049

Maoni of Wednesday, 10 November 2021

Columnist: www.tanzaniaweb.com

Aliyechora ramani ya mafanikio ya Liverpool huyoo anasepa

Michael Edwards aamua kuachana na Liverpool Michael Edwards aamua kuachana na Liverpool

Mkurugenzi wa ufundi wa Liverpool, Michael Edwards, amekataa kuongeza mkataba wake na klabu hiyo akisema anataka changamoto mpya.

Edwards ameitumikia Liverpool kwa takribani miaka 10 katika nafasi hiyo.

Alijiunga na klabu hiyo Novemba 2011, akiwa na wenzake wawili, Dave Fallows na Julian Ward ambaye atachukua nafasi Edwards.

Mwaka 2019 iliripotiwa kwamba Liverpool iliilipa Manchester City pauni milioni moja, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 2.8 kumaliza kesi nje ya mahakama kutokana na makosa ya kimtandao waliyoifanyia klabu hiyo.

Malipo hayo yalitokana na malalamiko ya Manchester City kwamba mfumo wao wa mtandao wa kompyuta wa kusaka vipaji na taarifa za kiufundi za timu na wachezaji, ulidukuliwa.

Makubaliano hayo ya siri ya nje ya mahakama, yalifanyika Septemba 2013 baada ya City kuwaajiri wataalamu wa kuchunguza udukuzi wa mitandao ya kompyuta, kuangalia kama kweli mtandao wao ulidukuliwa.

Tukio la makubaliano hayo lilitokea mwaka mmoja baada ya wasaka vipaji watatu wa zamani wa Manchester City kuhamia Liverpool.

Watu hao, akiwemo Michael Edwards, ambaye ndiyo huyu anayeseondoka, walituhumiwa na Manchester City kuhusika na udukuzi huo kwa kuingilia mfumo wa taarifa za kiufundi, zaidi ya mara 100.

Wawili waliobaki ni Dave Fallows, ambaye sasa ni mkuu wa kitengo cha usajili, cha Liverpool na Julian Ward ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Edwards na ndiye atakayechukua nafasi.

Edwards na wenzake walifanya kazi na Man City halafu wakahamia Liverpool na kuanza kuihujumu klabu yao ya zamani.

Waliiba ramani ya mafanikio ya Manchester City na kuihamishia Liverpool, na ndiyo iliyosabanisha mafanikio yote haya ambayo Liverpool imetayapata miaka ya karibuni.

Bila shaka Ward ambaye ni mmoja wa wale wadukuzi, atakalia kiti cha Edwards na kukitendea haki.

Tetesi zinadai kuwa Michael Edwards anakwenda kujiunga na New Castle United iliyo chini ya mabilionea wapya lakini mwenyewe amekanusha taarifa hizo.