Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 10 26Article 565987

Maoni of Tuesday, 26 October 2021

Columnist: www.tanzaniaweb.com

Asante kwa zawadi ya Manula Nienov

Aishi Manula akiwana aliekuwa kocha wa Makipa Simba, Milton Nienov Aishi Manula akiwana aliekuwa kocha wa Makipa Simba, Milton Nienov

Simba wamelivunja benchi lao la ufundi mchana wa leo. Wameachana na kocha mkuu, kocha wa viungo na kocha wa makipa. Kwangu sio stori mpya. Nilitarajia hili kutokea baada ya Mnyama kulala kwa Jwaneng Galaxy Jumapili jioni pale kwa Mkapa.

Sikuona kama kutakuwa na usalama kwa kocha Da Rosa, lakini sijajua kama kocha wa viungo na kocha wa makipa watakuwa sehemu ya Wahanga. Huyu kocha wa makipa anaondoka nchini kama shujaa kwetu Watanzania. Kuna sehemu amemfikisha kipa wetu namba moja wa Tanzania Aishi Manula.

Aishi amewahi kuwa chini ya makocha mbalimbali wa makipa nje na ndani na kuna sehemu makocha hao wamemfikisha, lakini huyu aliyeondoka Simba kuna sehemu amemfikisha zaidi. Hajamuacha Aishi kama alivyomkuta. Achana na makosa ya mechi ya Galaxy, kuna kazi kubwa kocha huyu ameifanya na Aishi katika kiwanja cha mazoezi pale Bunju na viwanja vinginevyo.

Kutajwa katika kapu moja na kina Mohamed Elshanawy, Dennis Onyango, Sherif Ekramy na wengineo sio kazi ndogo. Ni kazi ngumu. Kina Mwalami Mohamed 'Shilton' Iddy Abuubakar, Juma Pondamali 'Mensah', Saleh Machupa, Patrick Mwangata, Ivo Mapunda wamempa kitu Aishi, lakini huyu kocha aliyetimuliwa amemtoa eneo moja kwenye career yake na kumpeleka eneo lingine (Hii haina maana wakina Shilton hawajafanya kitu katika career ya Aishi).

Lakini chini ya kocha huyu Aishi ameimarika kwa kiasi kikubwa. Aishi wa sasa hadaki tena kizamani katika ile kudondoka dondoka tuliyoizoea kwa makipa wetu wengi nchini. Anadondoka inapotakiwa.

Hapotezi muda kipuuzi. Kuna makipa wanaamini ili uonekane kipa mahiri ni lazima ujidondoshe, huku wengine wakipenda kupoteza muda wakiamini ni mbinu ya mchezo.

Aishi ameshatoka eneo hilo la kuwa kipa wa kujidondosha hovyo na kupoteza muda kipuuzi puuzi.