Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 10 28Article 566452

Maoni of Thursday, 28 October 2021

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz

Hawafai, waamuzi machizi

Hawafai, waamuzi machizi Hawafai, waamuzi machizi

MICHEZO mingi iwe ya kirafiki au ya mashindano husimamiwa na waamuzi kwani kutokuwapo kwao kunaweza kutokea wachezaji, viongozi na hata mashabiki kutokubaliana na kusababisha vurugu. Hivyo ndivyo ilivyo katika kandanda, lakini ipo michezo ambayo mwamuzi badala ya kuhakikisha hakuna vurugu kwenye mchezo husika huwa chanzo cha kuleta mtafaruku ndani na nje ya uwanja.

Kwa kawaida, katika mchezo wa mpira wa miguu walio na mamlaka na madaraka ya kufunga au kuzuia bao lisitingishe wavu ni kipa, walinzi, wachezaji wa kati na wa mbele, lakini sio mwamuzi, wasaidizi wake au mtu yeyote aliyepo nje ya uwanja.

Lakini yapo mambo waliyofanya baadhi ya waamuzi wa kandanda ambayo unaweza kusema ni mikasa ya aina yake ambayo haikutegemewa. Kwa mfano mwaka 1981 ulikuwepo mchezo wa ligi uliokuwa na vuta nikuvute England kati ya timu ziliokuwa na uhasama mkubwa, Hull City na Huddersfield Town.

Mchezo huo ulikuwa unakaribia kumalizika na timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1. Mchezaji wa Huddersfield alisukuma mpira golini, lakini ilionekana wazi kwamba ulikuwa unatoka nje.

Mpira ulimgonga mwamuzi kwenye paja na kumbabaisha kipa na kwenda kutikisa nyavu. Mwamuzi alishikilia kuwa lilikuwa bao safi na kueleza kwamba ilikuwa ni bahati mbaya kwamba mpira ulimgonga na kuwataka wachezaji na mashabiki wa Huddersfield kulikubali bao la bahati mbaya.

Lile bao lililofungwa na mwamuzi liliipa Hull City ushindi wa mabao 2-1 na kusababisha Huddersfied kushindwa kupanda Daraja la Kwanza kwa vile walihitaji angalu kwenda sare ili kukata tiketi ya kucheza hilo msimu uliofuata.

Mwezi Septemba 2001, Brian Savill alikuwa mwamuzi wa Kombe la Bromley kati ya Earls Colne na Wimpole 2000 nchini Ujerumani. Savill, ambaye baadaye alisema alisikitishwa kuona Wimpole 2000 walikuwa wanaonewa na wapinzani wao na kuamua kuwahurumia angalau nao wawe wametikisa nyavu za wapinzani wao.

Mpira ulipodunda tu karibu yake alisukuma kombora la juu ambalo kipa alishindwa kulizuia. Alijipulizia filimbi kuwa ni bao na kuamuru uwekwe kati. Hata hivyo, hilo bao la sadaka ya mwamuzi halikuwasaidia Wimpole 2000 ambao walitoka uwanjani wakiwa wamefungwa mabao 20-2.

Mwezi mmoja baada ya kituko hicho Savill alijiuzulu baada ya kutakiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani kufanya hivyo au angefukuzwa kazi ya kuwa mwamuzi. Tangu wakati huo panapotokea timu kufungwa mabao mengi Ujerumani utasikia mashabiki wakipiga kelele za kumtaka Savill aende kusaidia.

Mwezi Mei 2019 kule Uholanzi mwamuzi Maurice Paarhuis aliifungia bao HSV Hoek dhidi ya Harkemase katika kinyang’anyiro cha mpira wa kona, lakini juu ya hilo matokeo yalikuwa Harkemase kuibuka na ushindi wa 4-3.

Uturuki nayo ilikuwa na mkasa wake 1986, ambapo mwamuzi Ahmet AkÁay aliyekuwa anachezesha pambano la ligi kati ya MKE Ankarag¸c¸ na Besiktas alijikuta na mpira karibu na bao. Bila ya kusita akaushindikiza wavuni na kusema hilo lilikuwa goi safi na Ankarag¸c¸ wakaibuka washindi wa bao 1-0.

Baada ya mchezo mwamuzi alisema alikuwa anawashangaa watu waliokuwa wanasema bao alilofunga si halali. Mwaka 1983 kulikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Brazil kati ya Santos na Palmeiras, ambapo mwamuzi JosÈ de Assis Arag„o alijikuta akifunga bao lililoisaidia Santos kupata ushindi wa mabao 3-1.

Mpaka dakika ya 90, Santos ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1, lakini dakika ya pili ya muda wa nyongeza mwamuzi huyo Arag„o kwa bahati mbaya alifunga bao hilo na kuibua hasira kwa mashabiki wa Palmeiras.

Aragio alipolaumiwa alisema: “Lolote linaweza kutokea katika mchezo kandanda. Ni muhimu kwa wachezaji na mashabiki siku zote kuwa wavumilivu. Kama huna uvumilivu kaa mbali na mchezo wa kandanda.”

Haya ya waamuzi si madogo hata kidogo. Sijui hali itakuwaje hapa Tanzania wakitokea waamuzi wa aina hii na kufanya madudu kama haya katika michezo yenye upinzani mkali. Tuombe tusiwe na waamuzi wa aina hii.

IMEANDIKWA NA SALIM SAID SALIM