Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 10 22Article 565027

Maoni of Friday, 22 October 2021

Columnist: www.tanzaniaweb.com

Hazina ya baadae kwa Taifa

Abdul Suleiman Sopu Abdul Suleiman Sopu

Kwa bahati mbaya sana macho yetu mashabiki yanaishia Simba na Yanga, zaidi ya hapo hatuhusiki, hatutaki kujua na wala hatujali.

Baada ya mjadala mrefu wa tuzo, ipo hii moja ya Abdul Suleiman Sopu ambayo kila mtu ameifumbia macho. Nadhani ni kwasababu tu hayupo Simba au Yanga

Sopu amechukua tuzo ya mchezaji bora kijana ambayo kwa maoni yangu mimi amestahili kwa asilimia zote.

Abdul Suleiman Sopu ni mmoja kati ya 'makumi' ya vijana waliopita timu za vijana za taifa. Hapa kama taifa tuna cha kujipongeza kwa kufanikiwa kulinda kipaji na kuna cha kutia moyo kwamba tunaelekea katika uelekeo usahihi.

Abdul Suleiman anacheza katika eneo ambalo tuna tatizo kubwa kama nchi. Eneo la kiungo wa uchezeshaji kuja mbele ni eneo ambalo kama taifa tumekwama kupata wachezaji wa kutosha ndiyo maana wageni wengi wanaokuja nchini wanakuja kucheza maeneo hayo.

Hawa akina Sopu ndio wazawa tunaowategemea kuja kung'aa katika eneo la hilo. Kwa miaka michache niliyomfahamu Abdul Sopu tangu Ndanda, Ngorongoro Heroes na sasa Coastal Union, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa.

Kikubwa anachohitaji ni kujilinda, kuzidi kupambana na kuwa na ndoto kubwa zaidi ya ligi kuu. Kucheza Sumba na Yanga haipaswi kuwa ndoto kubwa kwa vijana wa Tanzania. Kumbuka Novatus alichukua hii tuzo ya mchezaji bora kijana na leo yupo wapi??