Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 07 04Article 545194

Maoni of Sunday, 4 July 2021

Columnist: dar24.com

Hongereni "WANANCHI" Hongereni "WANAJANGWANI"

Yanga vs Simba Yanga vs Simba

A. Zawadi Mauya

Aliweza kutumia vizuri second ball na kuipatia Yanga bao la kuongoza. Comb yake na Mukoko ilikuwa sahihi.

B. Yacouba Songne

Hakuwa tu na bahati ya kufunga. Muda mwingi Tuisila, Kaseke na Feisal walikuwa wakimtengenezea nafasi za wazi. Kwa nyakati tofauti aliweza kuongeza presha langoni mwa Simba.

C. Mukoko V Feisal

Simba wana viungo wepesi ambao wanaweza kukuadhibu kwenye OPEN SPACES. Utulivu wao uliweza kuziba njia zote na kuwafanya Miquissone, Morisson na Chama kushindwa kufanya lolote lile.

D. John Bocco

Gomes alianza na mfumo wa 4-2-3-1 kamakawaida. Bocco alisimama kama mshambuliaji wa mwisho mbele, mara zote tunategemea mipira imfikie ili afanye maamuzi mazuri kwao lakini haikuwa hivyo