Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 09 17Article 558043

Maoni of Friday, 17 September 2021

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz

INGWE: AUSSEMS HAJATUTOKA, HIZO NI MASTORI TU

INGWE: AUSSEMS HAJATUTOKA, HIZO NI MASTORI TU INGWE: AUSSEMS HAJATUTOKA, HIZO NI MASTORI TU

UONGOZI wa AFC Leopards umekana tetesi kuwa kocha wao Mbelgiji Patrck Aussems kawafanyia umafia na kuwatoka kimya kimya.

Aussems aliondoka nchini mapema Agosti ligi ikiwa imesalia na mechi tatu kufika mwisho, na kuelekea kwao kwa ajili ya likizo.

Lakini mara tu baada ya kuondoka kulizuka madai kuwa klabu kadhaa ikiwemo Police FC ya Rwanda zilikuwa zikimvizia.

Hata hivyo uongozi wa Ingwe ulikanusha madai hayo huku Aussems naye akikana na kusema kuwa bado yupo na AFC leopards.

Kocha huyo wa zamani pale Simba ya Tanzania alitarajiwa kurejea nchini kuendelea na majukumu yake wiki iliyopita lakini mpaka sasa hajawasili.

Hali hiyo kwa mara nyingine imezua tetesi kuwa jamaa harudi. Lakini kulingana na meneja timu wa Ingwe Tom Juma, madai hayo sio kweli.

"Nakukuhakikishia kuwa Aussems atawasili nchini leo Alhamisi ili kuanza maandalizi ya msimu ujao. Hayo mengine uliyoyaskia ni mastoriu tu." Juma kasisitiza.

Juma aidha kasema tayari timu yao ilishaingia kambini kuanzaa maandalizi ya msimu mpya huku wakiwa wanamsubiri kocha Aussems.

"Tulianza maandalizi yetu juzi Jumatatu kwa kuingia kambini pale Camp Toyoyo. Wachezaji wote walihudhuria isipokuwa straika Bienvenue Shaka nisiyejua aliko." Juma kaongeza.