Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 11 14Article 571159

Maoni of Sunday, 14 November 2021

Columnist: Mwanaspoti

KWAKO JESSE JOHN: Ukitaka kwenda peponi ukubali kufa, World Cup tuisikie tu!

Stars haina nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia Stars haina nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia

Niliwahi kuandika makala moja niliyoelezea ugumu wa kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia hususani kwa taifa letu. Ndani ya makala ile yenye kichwa ‘Kwenda Kombe la Dunia ni Ndoto’. Niliainisha wazi mambo mengi yatakayotuchelewesha kwenda huko ikiwa ni pamoja na kuwa hatuna misingi imara kuanzia kwenye klabu tulikomezwa na Usimba na Uyanga.

Hamasa za dakika ya mwisho za wadau na muafaka wa wachezaji kutoka Zanzibar ambapo upande huo wanalalamika kutopewa nafasi kubwa! Tunapaswa kujijenga kwanza kwenye maeneo mengi kama taifa.

Juzi timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilijiondoa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwakani zitakazofanyikia Qatar baada ya kufungwa nyumbani mabao 3-0 na DR Congo, huku Benin akishinda nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya Madagascar. Jumapili mechi za Kundi J ilizopo timu hizo litahitimishwa kwa Tanzania kuifuata Madagascar ugenini, huku DR Congo wakiwa wenyeji wa vinara wa kundi hilo pale Kinshasa!

Stars imepoteza kwa Mkapa ikiwa inastahili kufungwa kutokana na namna ilivyocheza ndani ya kiwanja na timu ilionekana wazi kuwa chini kuanzia kwenye mazoezi ya kupasha misuli moto kabla ya mchezo maarufu kama ‘warm-up’ ambayo haikuonekana kuwa active sana! Mastaa wa Stars walifanya warm up yao kama timu ambayo haijazoea joto la jijini Dar es Salaam na ingekuwa ngumu kuvumilia mchezo kwa dakika 90 kwa utimamu ule ule yaani ‘endurance’.

Ndani ya mchezo Stars ilianza mchezo kwa utulivu na mipango na dakika ya 2 tu Simon Msuva almanusura aifungie Stars, lakini mpira ule ukaenda nje na makosa mawili ya Stars kukosa mabao yakageuka faida kwa Congo ambao waliendelea kujengewa hali ya kujiamini na wachezaji wa Tanzania na wao walipopata nafasi moja tu Gael Kakuta akafunga bao la kustukiza sana akiwa kwenye kisanduku cha hatari.

Wakati timu yetu ikionekana walau inaweza kuokota chochote mwalimu alifanya mabadiliko ambayo hayakuendana na kasi ya mchezo na pengine ni badiliko la Mzamiru Yassin tu ndio lilionekana kuwa na nafuu kwa timu ila ilikuwa vyema Mzamiru kucheza na Novatus Dismass badala ya kumtoa Novatus ambaye alionekana bora kwa dakika nyingi uwanjani. Advertisement

Wakati anatolewa Kennedy Juma hapo ndipo maswali yalikuwa mengi kuliko majibu kwa sababu ni Kennedy huyu huyu alionekana anaweza kupambana vyema na wachezaji wa Congo DR hasa kutokana na maumbo yao, hata hivyo tunaheshimu ufundi ule wa kocha lakini ni rahisi kusema tulihukumiwa zaidi.

Daraja la wachezaji wa Congo ni la juu sana na tumeadhibiwa kwa kustahili na hakuna miujiza ya kufuzu. Tunapaswa kuwa na mipango ya muda mrefu kwa kuwekeza kwenye usasa katika mpira vinginevyo tutawalaumu makocha wetu wakati hawana machaguo mengi katika kikosi na ‘quality’ ya wachezaji wetu wengi ni ya kawaida. Tujipange upya ila juzi meli ilielemewa na mzigo ule.

Tumekuwa na hulka ya kushangilia mtoto kabla mimba haijaleta tija!! “Safari hii lazima twende AFCON” ama “hakuna wa kutuzuia QATAR”!

Mara baada ya sare ya ugenini na DRC “tumewaweza” wetu hawa, laini kabisa! Bila kujua na kuwaheshimu kwa viwango, wakati tunachekelea kama tulichekelea kuwafunga Namibia kwao hatujipangi, labda kuwaita matajiri kujitangaza kivingine kwa kuchanga pesa lukuki! Tunasahau kuwa wenzetu wanajipanga, husikii tajiri chuprichupri sijui katoa bilioni 1, wala shabash katoa ndege! Hili nalo liangaliwe, inawezekana linawaondoa kisaikolojia mchezoni wachezaji wetu!! Mipesa kama yote hiyo ianze kujenga msingi katika klabu na hatimaye timu ya taifa.