Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 06 14Article 542500

Maoni of Monday, 14 June 2021

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz

KWAKO KASHASHA: Viungo namba nane hawa kiboko Ligi Kuu

KWAKO KASHASHA: Viungo namba nane hawa kiboko Ligi Kuu KWAKO KASHASHA: Viungo namba nane hawa kiboko Ligi Kuu

KUNA viungo wengi washambuliaji wanaocheza nafasi ya namba nane katika timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

Wapo ambao wamekuwa wakifanya vizuri, wenye viwango vya wastani na pia kuna wanaoshindwa kutoa mchango mkubwa kwa timu zao.

Wapo viungo wanne wanaocheza nafasi ya namba nane ambao kwa msimu huu wameonyesha kiwango cha kuvutia na wamekuwa na msaada mkubwa kwa timu zao.

Kwa kuanza nitaanza na kiungo wa Polisi Tanzania, Hassan Maulid. Kijana huyu licha ya jina lake kutokuwa kubwa sana na kama unavyofahamu Watanzania wengi tumekuwa hatufuatilii timu nyingine.

Polisi ina uwiano mzuri wa mechi za kushinda na kushindwa. Kijana huyu ni kiungo mshambuliaji mzuri na mahiri.

Kubwa zaidi ya yote ni mtulivu, ana ball control na anakuwa mahali popote kwa wakati sahihi, sio muoga na anajituma.

Pasi zake ni za uhakika na mara nyingi hazipotei na anaonekana ni box to box, ana discipline ya hali ya juu inayoendana na uwezo uwanjani pamoja na mbinu na ufundi.

Hana hasira, pamoja na battle za uwanjani huwezi kuona anahamaki na fair play kwake ni jambo la kawaida. Anaweza kuchezewa rafu akamuangalia mwamuzi na akafanya kile ambacho refa ameamua kwa haraka bila ubishani.

Mchezaji mwingine ni Feisal Salum wa Yanga. Kwa kipindi kirefu awali alikuwa anatumika kama namba sita lakini ukimuangalia typically ni kiungo mshambuliaji anapokea mpira, anapiga pasi, ana jicho la kuona goli na ana composure ya hali ya juu lakini pia ni mzuri sana wa kubadili uelekeo wa mpira.

Mara nyingi anapenda kupiga pasi fupifupi lakini anaweza kufunga mabao ya mbali. Passing discipline ya Feisal Salum ni ya kiwango cha juu. Passing accuracy ya maana na mara nyingi akipata mpira utaona timu imetulia hivi.

Football distribution yake ni nzuri. Mzuri katika kupiga diagnol passes na penetration passes. Ana uwezo wa kufika mbali zaidi iwapo ataongeza passion, bidii na kasi, ingawa kuna wakati amekuwa anacheza taratibu mno jambo linaloipa backline ya timu pinzani nafasi ya kusogea na kuwabana.

Ni mchezaji ambaye tayari katika ule umri amepata ukomavu na uzoefu wa kutosha kimataifa kupitia mechi za kimataifa na zile za Taifa Stars pamoja na timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ pindi inaposhiriki katika mashindano ya CECAFA Challenge.

Malengo yake ndio yatakuwa silaha kubwa zaidi ambayo itamfanya atoke hapa alipo na kwenda mbele zaidi. Inategemea na muendelezo na namna gani yeye mwenyewe atajielewa.

Kiungo mwingine ni Baraka Majogoro wa Mtibwa. Amekuwa na msimu mzuri, lakini bahati mbaya timu yake haikuwa na msimu mzuri. Siku akiamka vizuri mechi ikimkubali, anaweza kucheza ground na aerial balls na ball control yake ni ya kiwango kikubwa.

Ni mchezaji ambaye akiwa katika nafasi yake anatekeleza vyema majukumu yake kwa nafasi aliyopo. Amekuwa na uchu wa kupata mabao lakini ni mwepesi kuona wapi kuna gape wapi kuna njia na kupeleka mpira na ni mzuri sana katika one two.

Anapokuwa na mpira ni mwepesi sana kurespond. Akiwa kiwanjani utaona uhai wa eneo la katikati na hata Mtibwa wenyewe, mechi anayocheza inakuwa na ugumu eneo la katikati. Inaweza kufungwa lakini sio kwa uzembe wa eneo la kiungo.

Mchezaji mwingine wa mwisho ni Rally Bwalya wa Simba. Pamoja na ujio wake wa karibuni aliingia taratibu lakini ameonekana kuzoea mazingira.

Ana speed, anapiga na ni mzuri katika connection ya mpira ya kumaliza. Anaweza kuondoka katika msitu wa walinzi hata kama wako wengi.

Mzuri anajua namna ya kuondoka hata kama amedhibitiwa na watu wengi. Ana Discipline, sio mkorofi, anapenda kucheza na mpira na amekuwa ni msaada sana kwa timu ya Simba.

Ana jicho la kujua wapi apeleke mpira, movement na positioning yake uwanjani imekuwa ikiwapa wakati mgumu viungo na mabeki wa timu pinzani

Ni mchezaji wa kimataifa ambaye ana umri mdogo na kama akicheza bila kupata injuries uzoefu utazidi. Hatumii nguvu kubwa zaidi.

IMEANDIKWA NA ALEX KASHASHA