Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 05 26Article 539938

Maoni of Wednesday, 26 May 2021

Columnist: www.habarileo.co.tz

Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto zitokomeze ukatili

Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto zitokomeze ukatili Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto zitokomeze ukatili

SERIKALI imeanzisha jitihada mbalimbali za kutokomeza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto kwenye ngazi za mamlaka za serikali za mitaa, ikiwamo kamati ambazo zitawajibika kutoa ulinzi kwa makundi hayo.

Uanzishwaji wa kamati hizo una lengo la kuhakikisha utekelezwaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18 hadi 2021/2022 unatekelezwa ipasavyo.

Kimsingi masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto ni kati ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini, licha ya mpango huo wa kitaifa kuanza kutekelezwa tangu mwaka 2017.

Ukatili ni kati ya matukio ambayo yamekuwa yakijenga picha mbaya kwa jamii palipotokea vitendo hivyo, lakini pia yakimuumiza mtendewa, hivyo kwa namna moja hadi nyingine vinapaswa kupigwa vita.

Ukatili unaweza kumuumiza mtendewa kisaikolojia na kuharibu mfumo mzima wa maisha yake, waathirika wengine wakichomwa moto, kukatwa viungo vya mwili, kunyimwa haki za msingi kwa watoto ikiwamo shule, chakula na hata haki ya kupata matibabu.

Vitendo vya ukatili vipo vya aina mbalimbali, waathiriwa wengi wakiwa ni wanawake na watoto, lakini pia jinsia zote zikihusika kufanya vitendo hivyo kwa njia moja hadi nyingine.

Akijibu swali bungeni, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis amesema ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii, serikali ilianzisha kamati 16,343 ambazo zipo katika mamlaka za serikali ya mitaa.

Kamati hizo kwa zipo karibu zaidi na jamii, zitasaidia kufahamu wanafanya vitendo hivyo na hata waliofanyiwa na kushindwa kutoa taarifa kutokana na hofu au woga.

Wapo wanawake wanaouawa kikatili kwa

sababu mbalimbali ikiwamo kuongezeka kwa wivu wa mapenzi, wengine wakiuawa kwa sababu za hasira, wengine wakipigwa hata kukatwa viungo na wengine hata kuchomwa moto.

Ni matukio ambayo jamii imekuwa ikiona wenzao wakifanyiwa pengine wakishindwa kuchukua hatua kutokana na mfumo wa maisha ya Watanzania, ikiwamo kuyamaliza kwa ngazi ya familia bila kutambua kuwa kwa namna moja inasababisha vitendo hivyo kuendelea kuwapo.

Aidha, watoto pia ni kundi llinaloathirika na vitendo vya ukatili na pengine kutokana na kushindwa kujitetea, wakiumizwa kwa namna moja au nyingine, ambapo kamati hizo zinatakiwa kuhakikisha vitendo hivyo katika jamii vinatokomezwa ili kuwa na jamii yenye upendo na kujaliana.

Ni vyema kamati hizo zikaweka mikakati katika ngazi za mitaa namna ambavyo wanaweza kuifikia jamii inayowazunguka na kuhakikisha wanapata picha halisi ya kuwapo kwa vitendo hivyo na kuchukua hatua za kuyamaliza na kuiacha jamii ikiwa salama na amani.

Kuundwa kwa kamati hizo ni katika kuhakikisha kuwa, waliopo katika kamati hizo wanashirikiana na serikali za mitaa na wanajamii ili matukio hayo kwa wanawake na watoto yatokomezwe, lakini pia yasiwe ni chanzo cha kuzalisha chuki inayoweza kufikia kiwango cha kulipiza kisasi kwa jamii husika.

Kwa kuzingatia kuwa kamati hizo zimeanzishwa kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa katika jamii, zinatakiwa kufanyakazi usiku na mchana kumaliza tatizo hilo na kuacha alama.

Join our Newsletter