Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 12 18Article 579523

Maoni of Saturday, 18 December 2021

Columnist: Dk. Levy

Kuna Mondi, Kuna Wabongo

Staa wa ngoma ya Staa wa ngoma ya "unachezaje", Diamond Platnumz

Mondi katoa ngoma inaitwa ‘Unachezaje’. Wabongo kama hawajaelewa. Wakiamini iko chini ya kiwango stahili cha ‘Mondi Bin Laden’ wao. ‘Komenti’ za huko ‘insta’ zitakupa picha kamili.

Tatizo ni kwamba ‘Mondi’ na Wabongo ni vitu viwili tofauti. Wabongo wanaamini Mondi ni mali yao na wanataka awalishe watakacho lakini kiuhalisia anatakiwa kuilisha dunia.

Diamond Platnumz mnayemtaka yupo kwenye ‘kolabo’ za kina Zuchu. Kasikilize ‘vesi’ yake kwenye ‘Kwangwaru’ na Konde Boy. ‘Litawachoma’ au ‘Cheche’ na Zuchu. Yule ndiye Mondi wa Wabongo.

Mondi wa sasa hawezi kutoa wimbo kwa kuitazama Maneromango na Ubena Zomozi. Pengine hili ndo linafanya tusimuone Mondi yule wa ‘Ukimuona’ au ‘Mawazo’.

Mondi ni mali ya uso wa dunia hii. Vigumu kuimba kitu kama ‘Nitarejea’ na ‘Mbagala’ utegemee huko Gambia au visiwani Mayote wamuelewe.

Wa sasa ni wa midundo na mtiririko mtamu wa maneno. Hii hufanya hata asieelewa lugha basi afurahie midundo na ‘melodi’. Katika hili hahitaji kushikiwa bunduki kuelewa.

Mtu ambaye miezi miwili iliyopita alikaa meza moja na Nguli wa muziki Duniani Snoop Dog, Busta Rhymes na Swiss Beat, Wakijadili muziki halafu leo asijue ngoma ya kuachia?

Ukimtaka Mondi wa ‘Nenda Kamwambie’ na ‘Ukimuona’ subiri ‘kolabo’ yake na Linex ama Ben Pol, lakini ngoma zake binafsi kwa sasa ni kama ile ‘Parakatatumba’.

‘Kolabo’ yake na Davido ya ‘Number One remix’. Ilikuwa kama ‘roho kuacha mwili’. Kuanzia hapo mtazamo wake ulikuwa wa kidunia na siyo ‘Mongolandege’.

Usishangae hili goma likabamba na kubeba tuzo. Kwa sababu muziki wa dunia siyo ujumbe tu, bali ni kelele zilizopangiliwa vizuri.