Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 05 22Article 539110

xxxxxxxxxxx of Saturday, 22 May 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MZEE WA MCHANGANI: Mukoko, Chama nusura wazichape

Kazi ya mwanaume hapewi mtoto! Ndiyo maneno ya mashabiki wa Chiba FC baada ya nyota wao maarufu kama Mukoko kutaka kuzichapa na nyota wa Boli Mkwanja maarufu Chama kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa wiki hii katika Dimba la Chamazi shule ya msingi.

Ilikua patashika nguo kuchanika katika mchezo huo dakika kama ya 25 hivi kipindi cha kwanza ambapo Chama wa Boli Mkwanja alimpiga chenga Mukoko na kumpita jambo ambalo lilimjaza upepo Mukoko na kwenda kumchezea faulo iliyoonekana ya makusudi.

Ebwana eeh! Chama akahamaki, wakaanza kushikana jezi hadi mwamuzi akaingilia kati na kuamua wote wawili watoke nje ya uwanja mpaka pale atakapowaita tena.

Mashabiki wa Chiba FC nje ya uwanja waliendelea kulalamika huku wengi wakisema refa anampendelea Chama dhidi ya Mukoko kutokana na umbo lake dogo.

“Huyu dogo (Chama) anabebwa sana, anapiga chenga zake za kitoto na kila akiguswa refa anapuliza filimbi, hili ni soka kama hataki mchezo wa kugusana basi akacheze bao au karata,” alisema shabiki mmoja wa Chiba FC.

Baada ya dakika kadhaa kupita mwamuzi wa mechi hiyo aliamuru Chama na Mukoko kurejea uwanjani na soka kuendelea huku upinzani wao ukionekana kuwa mkubwa hadi dakika 10 kabla ya mechi kumalizika Chama alipofanyiwa mabadiuliko.

Pamoja na presha ya Chama na Mukoko kati kati ya kiwanja lakini mechi hiyo ilimalizika kwa suluhu (0-0) na baada ya mechi kila timu ilisepa kivyake.

Join our Newsletter