Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 09 13Article 557128

Maoni of Monday, 13 September 2021

Columnist: BBC Swahili

Mabadiliko Baraza la Mawaziri yanatoa taswira ipi katika siasa ya Tanzania?

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Miongoni mwa teuzi kubwa zilizokwisha fanyika. Ni uteuzi wa Mabalozi wapya Mei 23, 2021. Juni, 2021 kulifanyika uteuzi wa wakuu wa wilaya.

Shughuli imeendelea kwa kufanyika uteuzi uliobadilisha kidogo sura ya Baraza la Mawaziri siku ya jana. Mawaziri wanne wamepewa majukumu, wawili wakiwa wanawake na wawili wanaume. Pia kumefanyika uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Haya ni mabadiliko madogo ya pili ya baraza hilo tangu kifo cha Rais John Pombe Magufuli March 17, 2021. Mabadiliko ya kwanza yalifanyika Machi, 2021 Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati wa hafla ya kumuapisha makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Uwiano huu wa kijinsia katika uteuzi wa Mawaziri wa sasa, unaakisi pakubwa ahadi ya Rais Samia ya kuleta usawa wa kijinsia katika nafasi za kiungozi. Ingawa safari bado inaweza kuwa ni ndefu kufikia usawa wa hamsini kwa hamsini.

Msomi wa mawasiliano ya Teknolojia ya Habari na mwanasiasa Profesa. Makame Mnyaa Mbarawa, ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Akichukua nafasi ya Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Ukosoaji makubwa ulisikika wakati wa uteuzi wa Baraza la Mawaziri chini ya Hayati John Pombe Magufuli, Disemba 2020 baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba wa mwaka huo. Ukosoaji ulitokana na kukosekana Waziri kamili kutoka upande wa Zanzibar.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo kwa misingi ya Muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar. Hivyo, naamini Serikali inaundwa ina wajibu wa kuwa na Baraza la Mawaziri lenye kuakisi sura ya Muungano.