Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 10 13Article 563041

Maoni of Wednesday, 13 October 2021

Columnist: mwananchidigital

Maswali tata uchaguzi wa marudio jimbo la Konde

Maswali tata jimbo la Konde Maswali tata jimbo la Konde

Ni maswali katika Jimbo la Konde ambalo ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja, wananchi wake wamefanya uchaguzi wa ubunge mara tatu, huku wakishuhudia wagombea watatu wakishinda na wawili kupishana kwa idadi ya kura ndani ya miezi miwili.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2020, Khatibu Said Haji wa ACT-Wazalendo aliibuka mshindi kwa kupata kura 1,552 akiwashinda wagombea wa CCM, Sheha Mpemba Faki aliyepata kura 1,245, Masoud Othman Bakari (Ada-Tadea) aliyepata kura 18, Bakar Makame Khamis (ADC) aliyepata kura 38, Mohamed Suleima Said (Chadema) aliyepata kura 781, Omar Hamad Khamis (CUF) aliyepata kura 92, Abrahman Mbarouk Juma (Demokrasia Makini) aliyepata kura 26 na Abdirahim Ali Slum (NCCR-Mageuzi) kura 59.

Hata hivyo, Khatib alifariki dunia Mei 2021 katika hospitali ya Taifa Muhimbili na jimbo hilo kubaki wazi kabla uchaguzi mdogo kufanyika Julai 18, mwaka huu na Sheha Faki Mpemba (CCM), kutangazwa kuwa mshindi, lakini akajiuzulu kabla ya kuapishwa kwa madai ya familia yake kutishiwa maish

Matokeo ya uchaguzi huo yalidaiwa kutikisa siasa za Zanzibar, hasa baada ya ACT-Wazalendo kudai kuwa mgombea wao, Mohamed Said Issa ndiye aliyeshinda.

Baada ya kujiuzulu kwa Faki, Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud alisema kada huyo kajiuzulu baada ya yeye (Othman) na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Mwinyi kuhusu dhulma iliyofanyika kwenye uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo, Mpemba alishinda kwa kupata kura 1,796 dhidi ya Mohamed Said Issa aliyepata kura 1,373 kati ya kura 5,050 zilizopigwa.