Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 12 16Article 579004

Maoni of Thursday, 16 December 2021

Columnist: www.mwananchi.co.tz

Miaka 60 ya uhuru na uwekezaji nchini

Miaka 60 ya uhuru na uwekezaji nchini Miaka 60 ya uhuru na uwekezaji nchini

"Tangu mwaka 1961, Tanzania imekuwa ikianzisha sera, sheria, taratibu, kanuni, mipango, na mikakati mbalimbali kufanikisha uwekezaji nchini," anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu I. Kazi.

Ili kufikia azma hiyo kwa makusudi mwaka 1963 serikali ilianzisha sheria ya Uhamasishaji Uwekezaji wa Nje No. 40 (The Foreign Investment Protection Act No: 40 of 1963), ikifuatiwa na Azimio la Arusha (Nationalization Act of 1967) ambalo lililenga kuinua uchumi kupitia Sera za Ujamaa na Kujitegema.

Serikali pia ilianzisha sheria ya Uhamasishaji na Ulinzi wa Uwekezaji ya 1990 (National Investment Promotion and Protection Act of 1990), Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya 1996 (National Investment Policy 1996), Sheria ya Uwekezaji ya 1997 (Tanzania Investment Act of 1997) iliyo anzisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania.

Kituo cha Uwekezaji ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya Sheria Na. 26 ya mwaka 1997 ikiwa na majukumu ya kuhamashisha na kuwezesha Uwekezaji Tanzania. Aidha, Kituo kinaishauri Serikali kuhusu Sera na masuala yanayohusu Uwekezaji.

Kituo pia kimepewa jukumu la kuanzisha na kuwezesha juhudi zitakazoboresha mazingira ya uwekezaji nchini, kukusanya na kusambaza taarifa kuhusu fursa za uwekezaji na kushauri wawekezaji kulingana na maombi kuhusu uwepo wa wabia kwenye miradi ya ubia, kuainisha maeneo ya uwekezaji, au ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Mafanikio

Advertisement Moja ya mafanikio katika eneo la uwekezaji katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru ni kuanzishwa kwa Kituo cha kwanza cha Uwekezaji “Investment Promotion Centre (IPC)”, kilianzishwa mwaka 1990 chini ya Sheria ya Taifa ya Kuhamasisha na Kulinda Uwekezaji ya mwaka 1990 The “National Investment Promotion and Protection Act, 1990”.

Kituo kilipewa jukumu la kuhamasisha, kuratibu na kuthibiti na kufuatilia uwekezaji wa nje na ndani ya nchi. Kituo kilikuwa chini ya Ofisi ya Rais Tume ya Mipango. “The Centre operated under the President’s Office Planning Commission.”

Maeneo yafuatayo yalikuwa muhimu kimkakati na yaliachwa kwa ajili ya uwekezaji wa umma isipokuwa pale tu ambapo leseni maalum zilitakiwa kutolewa. Kituo kiliishauri Serkali maeneo ni uzalishaji bidhaa, masoko na usambazaji wa mapambo na milipuko ya aina zote, uzalishaji na usambazaji umeme katika miji, au kupitia gridi ya Taifa, utoaji wa maji ya umma kwa matumizi ya nyumbani na matumizi ya viwanda.

Pia kujenga na kuendesha reli, redio na televisheni, pia ujenzi na usimamizi wa shirika la Reli, kurusha matangazo Redio na televisheni, posta na huduma za mawasiliano ya simu, (na uzalishaji wa vifaa), bima na huduma za bima na mabenki.

Kwa upande mwingine, maeneo yafuatayo yalipangwa kwa ajili ya wawekezaji wa ndani (Watanzania) pamoja na biashara ya jumla na rejareja, udalali wa bidhaa, uwakilishi wa bishara ya makampuni ya nje, kuendesha shughuli za biashara ya umma, taxi, saluni za kunyoa nywele, saluni za urembo na maduka ya nyama.

Uanzishwaji wa Sera na Sheria mbalimbali ikiwemo Sera ya Uwekezji Tanzania 1996 na Sheria ya Uwekezaji Na.26 ya mwaka 1997 uliwezesha kuanzishwa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania mwaka 1997 kikiwa na majukumu ya Kuhamasisha na kufanikisha Uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya Uwekezaji.

Kuanzishwa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilianzishwa tarehe 1 Septemba, 1997 kwa Sheria ya Bunge Na.26 ya mwaka 1997.

Kituo hiki kiliundwa baada ya kufutwa kwa Kituo cha Kuhamasisha Uwekezaji (Investment Promotion Centre) iliyoundwa mwaka 1990.

Malengo makubwa ya kuanzisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre) pamoja na mambo mengine ni kuwa na taasisi mama ya Serikali ya Tanzania ya kuratibu, kuhimiza, kuhamasisha, kufanikisha na kuishauri Serikali kuhusu sera sahihi na mambo mengine yanayohusu uwekezaji.

Majukumu ya Kituo cha Uwekezaji yameainishwa na kufafanuliwa vizuri katika Kifungu cha 6 cha Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Sura ya 38.

Majukumu mengine ya Kituo cha Uwekezaji ni pamoja na Kuwahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye sekta na Meneno muhimu ya kimkakati yatakayokuza uchumi kwa haraka kama vile; Viwanda, Kilimo, Mifugo, Utali, Uvuvi, Madini, Rasilimali watu, Mafuta na gesi.

Maeneo mengine ya kimkakati ni pamoja na; Uanzishwaji wa miradi ya Kongani, Viwanda vya Kuchakata Vito ikiwemo Tanzanite, Uwekezaji kwenye huduma za afya na elimu, Ujenzi wa Textile city, ujenzi wa reli ya Kisasa, Mradi wa Liganga na Mchuchuma, pamoja na uchimbaji wa madini ya SODA ash.

Kuandaa na kusambaza taarifa sahihi kwa wawekezaji kuhusu fursa za uwekezaji pamoja na upatikanaji wa mitaji na wabia, kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati katika kuibua fursa za uwekezaji kwa lengo la kukuza biashara zao, kufanya tafiti za uwekezaji ili kuwekezesha kushauri maboresho ya mazingira ya uwekezaji.

Maboresho mbalimbali yaliyofanyika Kituo cha Uwekezaji yamewezesha Kituo kutwaa tuzo ya Kituo bora cha Uwekezaji Duniani kwa mwaka 2007 ‘The Best Investment Promotion Agency of the World 2007’ ikifungana na Kituo cha Uwekezaji cha nchini Ugiriki kati ya vituo vya Uwekezaji 184 ambavyo ni wanachama wa World Association of Investment Promotion Agencies (WAIPA) na kwa mwaka 2008 Kituo cha Uwekezaji kiliweza kushinda tuzo ya dhahabu kwa kuwa mshindi wa kwanza wa Innovative Management by the African Association for Public Administration and Management (AAPAM) 2008 iliyofanyikia Accra, Ghana kati ya taasisi 39 za serikali zilizoshindana Afrika.

Mafanikio hayo kwa namna moja au nyingine yalistua sana Washindani wa Kituo cha Uwekezaji (vituo/ IPAs za nchi jirani, na zilianza kuja kujifunza namna ya kuendesha Huduma za Dirisha la Pamoja hapa TIC, nchi zilizokuja ni Msumbiji, Malawi, Uganda, Rwanda, Zambia na Kenya.

Kutokana na washindani kujifunza na wengine kuchukua, namna ya uendeshaji dirisha la huduma la pamoja.

Uanzishwaji wa Mipango, Mikakati, Programu na taasisi mbalimbali za Taifa

Mwaka 2000 Serikali ilifanikiwa kuandaa dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo hadi sasa inatumika na mwaka 2020 Tanzania ilifanikiwa kuingia katika nchi za kipato cha Kati cha chini, kuanzishwa kwa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na kuanzishwa kwa Sheria ya PPP (yakiwemo masuala ya fedha na Uratibu –Finance and Coordination Unit).

Uanzishwaji wa Baraza la Taifa la Biashara

Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Serikali ilianzisha TNBC na Taasisi ya Maendeleo ya Sekta Binafsi TPSF na kutekeleza programu na mipango mbalimbali ikiwemo BEST, BRN (Kilimo Kwanza), SAGCOT 2011 baada ya Mkutano wa World Economic Forum, programu ya ASDP I na ASDP II, Blue Print: Serikali inaendelea kutekeleza Blue print ikiwemo kuunganisha baadhi ya taasisi au majukumu ya baadhi ya taasisi kwa mfano ili kuongeza ufanisi katika utendeji Serikalini.

Mfano TFDA na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), masuala ya viwango vya Chakula yaliyokuwa TFDA yalihamishiwa TBS na kupelekea TFDA kubadilika kuwa TMDA.

Fursa za uwekezaji mpya kutokana na miradi mikubwa ya kipaumbele

Kujengwa kwa miradi mikubwa ya Standard Gauge Railway (SGR), Julius Nyerere International Airport (JNIA) Terminal III, Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere llitakalozalisha umeme wa MW 2,115 ambalo litakuwa kubwa katika Afrika Mashariki na Kati kumeanza kuiibua fursa nyingi ambazo inabidi wawekezaji wa ndani na nje wazichangamkie. Kituo cha Uwekezaji kimeanza kuibua fursa hizo na kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza.

Uanzishwaji wa Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja: (One Stop Facilitation Centre-OSFC) zilianzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji Na. 26 ya 1997 ambayo iliweka utaratibu wa utoaji wa vibali, na leseni mbalimbali mahala pamoja ili kumrahisishia mwekezaji wa ndani na wa nje kupata vibali hivyo kwa urahisi zaidi.

Kifungu cha 16 cha sheria ya Uwekezaji, kinazitaka taasisi zote za Serikali kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji katika kutoa huduma hizo kwa wawekezaji.

Hata hivyo kituo kimefanikiwa kuwaleta pamoja Wizara na taasisi 12 ambazo ni Wizara ya Kazi (masuala ya vibali vya kazi), Wizara ya Ardhi (masuala ya Ardhi-Derivative rights), Idara ya Uhamiaji (Masuala ya vibali vya ukaazi, TIC (kuratibu na kutoa Cheti cha Vivutio), BRELA (Usajiri wa Kampuni), NIDA, TBS, NEMC, OSHA, TRA, TMDA na TANESCO.

Uanzishwaji wa Ofisi za Kanda

Kituo cha uwekezaji kilianzisha ofisi za kanda kwa lengo la kusogeza huduma zake karibu na wawekezaji. Ofisi hizi zilianzishwa katika kanda tatu za kanda ya mashariki, kanda ya ziwa na kanda ya nyanda za juu kusini.

Kwa sasa kituo kinatoa huduma zake katika kanda saba zikijumuisha kanda mpya zilizoanzishwa mwaka 2019 kanda hizo ni kanda ya mashariki, kanda ya kusini, kanda ya magharibi na kanda ya kati

Miradi iliyosajiriwa

Tangu mwaka 1997 hadi Oktoba 2021, Kituo cha Uwekezaji kimesajili, jumla ya miradi 11,365 yenye thamani ya Dola za kimarekani 809,042 ambayo ilitarajiwa kuzalisha ajira 16,459,885.