Uko hapa: NyumbaniWallMaoniArticles2020 03 26Article 498925

Maoni of Thursday, 26 March 2020

Columnist: mwananchi.co.tz

Siku 30 za mateso, shida na njaa kwa sanaa na wasanii

Siku 30 za mateso, shida na njaa kwa sanaa na wasanii

Alikuwa mrefu. Lakini siyo ule urefu wa kukera. Kuna urefu hupoteza mvuto machoni. Huyu alikuwa na urefu wa kuvutia. Urefu ambao huongeza mvuto wa kutembea, kugeuka au kuweka pozi la kupiga picha. Dem mrefu akipiga picha na kubinua mguu huvutia zaidi tofauti na mfupi. Mfupi akibinua mguu anakuwa kama chaja ya kobe.

Yupo kwenye ofisi ya shirika moja la umma lenye vinasaba na pesa. Nikalazimika kumfuata yeye ili anihudumie. Kadri nilivyomsogelea nikaona anashusha mikono chini ya meza. Kama mtu anayechukua kitu huku akinitazama kwa makini. Kwa taifa lingine ningehisi anachukua bastola, lakini tabasamu lake liliniondolea hiyo hofu.

Kadiri nilivyotuma hatua za miguu yangu kumkaribia. Ndivyo ambavyo mikono yake ilivyosogea usoni kwake. Akiwa na kitu cheupe ambacho alikifunga kuziba midomo yake mitamu (maski). Fahari ya kwanza kuitazama ambayo ni midomo ilitoweka. Nikakumbuka neno corona na kuzidi kuvichukia zaidi hivi virusi vya kiibilisi. Dah.

Dada alinihudumia huku sauti ikitokea ndani ya maski. Namna ubora wa ile sauti ilivyosikika nikawaza inakuaje akiwa hana maski mdomoni. Sauti flani hivi ambayo huondoa kabisa mawazo ya kifo moyoni. Kuna warembo huumbwa bila kasoro. Achana na misemo ya wahenga waongo wale. Eti kizuri hakikosi kasoro huyu alikuwa hana kasoro. Wahenga bana sasa kasoro ya huyu itakuwa kwenye kupika? Si naenda hotelini, kupika ni urembo? Jeuri? Sasa ataachaje kuwa jeuri na uzuri wote huu? Kwanza asipokuwa jeuri ina maana hajui thamani ya urembo aliyopewa na Muumba. Kuna misemo tuanze kuipuuza kama vijana. Matumizi yake yamepitwa na wakati kama demu mzuri ni mzuri tu.

Kwanza nilishangaa mrembo yule kufanya kazi ofisi ile. Bila hata kutegemea elimu, urembo wake tu hakutakiwa kuwa pale. Hastahili kukatwa eniesiesiefu, sijui taksabo inkamu wala payee. Ndo wale warembo ambao walikuja duniani kwa bahati mbaya tu. Alifaa kuwa peponi na kuwa mmoja wa wahudumu wa watakatifu.

Corona ilinikosesha fursa ya utalii wa ndani. Huu ni zaidi ya utalii maana ndani yake kuna burudani na kuongeza siku za kuishi. Kuna warembo hupaswi kuwaona nusu nusu. Baada ya kuhudumiwa na kugeuka ili niondoke. Ndipo nilipogundua kuna viumbe wengi waliovaa maski. Nilipotoka nje kitu cha kwanza kufanya ni kutafuta maski zinapouzwa.

Pia Soma

Advertisement
Moja ya kivutio kikubwa kwa totozi ni lipsi. Kwenu Namtumbo mnaita papi. Hivi sasa kinageuka kuwa kitu adimu. Kila mtoto mkali ana maski usoni kama zombie. Inakera. Tunaambiwa wanaotakiwa kuvaa ni wenye maambukizi, ila mbona kwenye tivii tunaona huko kila mtu kavaa? ‘Enewei’ nyie vaeni tu.

Najaribu kuangalia namna ambavyo watu wamepokea hii taarifa. Kifo si jambo zuri mwitikio wa watu jinsi ya kujikinga na corona ni mkubwa. Hapo ndo unakosa jibu kuona kuna watu wanajiua kisa mapenzi. Wanapata wapi huo ujasiri wakati kila mtu ni mwoga wa kifo namna hii? Ujasiri upo wa aina nyingi inategemea umefanya nini.

Kujiua ni ujasiri. Kama ambavyo ni ujasiri kwa yule mbunifu wa virusi vya Ukimwi kuendelea kuishi. Hivi unapata wapi ujasiri wa kuishi ukisifika kama mgunduzi wa virusi vya Ukimwi? Huu ni ujasiri mkubwa wa kiwango cha SGR. Miaka ijayo Mungu akitupa uhai tutashuhudia mahojiano ya mtengenezaji wa virusi vya corona. Tupo hapa.

Dunia hii imekusanya wehu wengi wa sifa tofauti. Wehu wa Iddi Amini na Adolf Hitler, ni ule ule wa hawa wagunduzi wa corona na HIV. Ndo maana ikawa dunia kwa kuwa na mkusanyiko wa kila kitu. Leo hii dunia nzima imetulizwa na virusi vya corona. Biashara zimesimama, elimu imesimama. Maisha yetu ya kawaida yako likizo bila malipo. Hili ni tatizo lenye tatizo.

Siku 30 bila mikusanyiko ina maana hakuna shoo kwa wasanii wote. Bahati nzuri tatizo limekuja wakati ambao hawategemei sana shoo. Hapo kabla waliendesha maisha yao kwa shoo na mauzo ya albamu. Leo hii wanategemea pesa za YouTube. Tatizo ni wasanii wangapi wana wafuasi wa kutosha? Hapa ndIo penye mtanziko Kwa sanaa na wasanii wengi.

Wachache wanaopiga pesa ndefu ya YouTube. Wengi huungaunga tu. Kama ambavyo shoo pia siyo wote hulipwa pesa nyingi. Wasanii ni wengi lakini wenye fursa za kupiga pesa ndefu ni wachache. Hili ni jambo la dunia nzima pesa anayolipwa Jay Z ni tofauti na ile anayolipwa T Pain. Lady Gaga ni tofauti na Alicia Keys. Iko hivyo na haikwepeki. Ndo maana wasanii hutumia kila njia ili ‘kutrendi’. Kadri msanii anavyotajwa sana kwa sanaa yake na nje ya sanaa. Ndivyo ambavyo dili nyingi husogea kando ya mlango wake. Tazama wasanii wanaopata dili za matangazo. Utapata jibu. Hupewi mchongo wa namna hiyo msanii ambaye huzungumziwi kwa hili wala lile.

Si hilo tu. Pia tuna uhakika gani kuwa hizo siku 30 tatizo litaisha? Likiendelea huko mbele kuna Fiesta na Wasafi Festival. Hizi ni shoo kubwa ambazo asilimia 90 ya wasanii wetu wanazitegemea. Ndo maana miezi michache kabla ya Fiesta utasikia matoleo mapya mengi ya singo mpya. Wanavizia wakati wake. Kuna mambo yanakuja kwa makusudi ili kuondoa au kuongeza kitu. Lakini kuna yanayokuja kwa lengo moja la kuharibu tu. Huu mchongo wa corona umekuja kwa lengo moja tu la kuua. Si jambo la kufanyia mzaha. Kama hautaathirika kwa corona, utaathirika kwa madhara mengine ya uwepo wa corona. Yes!

Watu tupo kwenye mbio na maisha ‘wei baki’. Kujilinda kwa kondomu, kujilinda kwa kofia ngumu kwenye bodaboda. Kinakuja kitu cha kindezi toka huko kinakotoka. Eti kinataka kutuondolea uhai kibwege kwa mtindo wa kugusana. Kuna vitu vinatumwa vibaya.

Kila siku tumekuwa watu wa hofu. Na haya hutokana na mwingiliano mkubwa sana kwa sasa. Dunia imekuwa kama mkusanyiko wa nywele kichwani. Tuliona kama mbali sana China walipolia. Tukaacha milango wazi huku tukitegemea vifaa vyetu pale JNIA tu. Leo hii hata mwaka haujaisha corona imetua kwenye ardhi yetu. Msala.

Waswahili wenyewe tuna mazoea mabaya. Salamu hadi tupeane mikono. Wengine mpaka wagusane mashavu. Wakati tunaendekeza hayo usafi kwetu ni mtihani. Kunawa mikono mpaka wakati wa kula ubwabwa au ugali. Ndo maana kipindupindu kikiibuka kila mwaka kinasepa na kijiji. Tuna tatizo.

Sawa kunawa kila wakati. Maji yenyewe kuyapata kwa mbinde. Kwa hiyo hatuna uhakika wa usafi. Hatuna uhakika na maji na hatuna uhakika na vifaa tiba. Tunaishia kumuachia Mungu. Kinachokera zaidi kuna akili mbovu zinageuza hili janga kama jambo la kufanyia mzaha na mazoea. Jambo ambalo mzungu linamtoa jasho?

Corona dunia ya tatu

Dunia inayotegemea matumizi ya pesa kwa keshi. Mrundikano wa wasafiri kwenye vituo vya usafiri. Nenda Kimara mwisho asubuhi, Gerezani Kariakoo jioni, Ferry asubuhi mchana na jioni. Kote huko kuna mafuriko ya watu kutegemea vyombo vya usafiri.

Nenda Mbagala Rangitatu asubuhi, Gongo la Mbogo asubuhi na Buguruni jioni. Watu wanagombea usafiri kila siku. Hata hizo maski hazina maana wakati mwingine. Tunalazimika kumuachia Mungu atulinde. Badala ya kuiachia sayansi ifanye kazi yake na serikali kutuwekea miundombinu sahihi. Kama huna cha kufanya nje, kaa ndani kwako.

Kitu ‘kinachotrendi’ kwa sasa ni corona. Wasanii tumieni kurasa zenu mitandaoni kuwaelimisha wafuasi wenu. Corona si kitu cha polepole wala kuchukulia poa. Kama mzungu katulizwa kibwege anashindwa aanzie wapi. Inakuaje sisi? Mkipuuza inaweza kuwa siyo siku 30 tena bali ikawa milele. Mtamuimbia na kumtumbuiza nani wote wakiwa wagonjwa?Join our Newsletter