Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 09 21Article 558820

Maoni of Tuesday, 21 September 2021

Columnist: TanzaniaWeb

Siri ya Diamond kuwa jeuri hii hapa

Diamond Platnumz Diamond Platnumz

NAOMBA nikufahamishe tu kwamba linapokuja suala la kuvaa, msanii Diamond Platnumz anautendea haki kikwelikweli huwa mwili wake, hafanyi kwa sababu ya kujifurahisha ama kufurahisha watu, lakini anafanya kwa ajili ya kuilinda brand yake aliyoitengeneza kwa zaidi ya miaka 10 sasa na kuendelea kuikuza zaidi na zaidi.

Sasa basi, kutokana na umaarufu wa nguli huyo wa muziki wa Bongo Fleva, tumeweza kumshuhudia akitoka na mavazi ya kila mitindo na yenye thamani kubwa, jambo ambalo linachoashiria kwamba utajiri wa msanii huyu ni wa hali ya juu.

Bila kupepesa macho, kwenye suala la kujipamba ni kwamba Mondi ni mtu ambaye anajijali sana. Kama utakumbuka wakati ametoka na vazi hili hapa ameonekana akipiga picha nyingi na gari lake jipya aina ya rose Royce na kuzisambaza kwenye mitandao yake ya kijamii na watu wake wa karibu.

Maisha ya Diamond yanabadilika siku hadi siku kulingana na thamani na umaarufu wake kuzidi kukua. Jamaa huyu ni nyota wa kipekee sana Bongo na Afrika Mashariki kwa sababu mafanikio yake hapa huwezi kuyafananisha na wasanii wengine nchini kwa sasa lakini pia Afrika ya Mashariki na Kati, hata kama utakataa lakini huo ndiop ukweli.

Utakubaliana nami kwamba, mwamba huyu tangu aanze rasmi kazi ya muziki amekuwa akipaa juu kila mwaka, hajawahi kushuka wala muziki wake kugonga mwamba. Kama tunavyojua, miezi michache iliyopita Mondi alitimiza ndoto yake ya kumiliki gari kali kwa kununua gari la mabilioni ya pesa linalojulikana kama Rose Royce ya mwaka 2021.

Lakini tangu amenunua gari hilo amekuwa akijiita jina la gari hilo yaani Mr Rose Rroyce. Unajiuliza, kwamba kwa nini ajiite jina hilo? Lakini yeye ndiye mwamzi na mwenye maana halisi.

Acha hivyo tu, Mondi amekuwa msanii wa mfano wa kuigwa kwa watu wengi hapa Bongo na dunianiu kutokana na wamba amekuwa akiwa-inspire vijana walio wengi kufanya muziki wa ushindani na biashara ili kuyafikia malengo yao, wengi amekuwa akiwatia moyo na wanatamani kuwa kama yeye, kitu ambacho kinawafanya kupambana usiku na mchana.

Umiliki wa lebo yake ya WCB

Yeye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lebo ya WCB Wasafi Record, Zoom Extra, Wasafi TV, chombo cha habari cha Tanzania, na Wasafi Fm.

Haya yanaonesha ni kwa jinsi gani mtu huyu alivyo wa kipekee na aliyeweza kufikia mafanikio makubwa sana na ukizingatia ni kwamba bado ana umri mdogo yaani umri wa kawaida sana. Hivyo mpaka sasahivi ni mmojawapo ya matajiri wakubwa nchini na duniani.

Diamond ni miongoni mwa wasanii wakubwa Afrika Mashariki na Kati wanaopata mapato makubwa katika tasnia ya muziki.

Mnamo 2021, Diamond pamoja na lebo yake ya WCB Wasafi waliingia katika ushirikiano na Kikundi cha Muziki cha Warner. Lengo kubwa likiwa ni kupanua soko la muziki na kudumisha uhusiano mzuri hasa wa kibiashara baina ya Tanzania na Afrika ya kusini.

Dini na mahusiano ya kifamilia ya Diamond Platnumz

Ikumbukwe kuwa, malkia wa Filamu Bongo, Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii waliosaidia kwa kiasi kikubwa kulitangaza jina la Mondi baada ya kuanzisha naye mahusiano yaliyokuwa yakizungumza kila kona kutokana na umaarufu wa mwanadada huyo aliyewahi kutoka na Steven Kanumba.

Baada ya kuachana na Wema, mwishoni mwa mwaka 2013, Mondi aliingia katika mahusiano na mwanadadada mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda, Zari the Boss Lady ambaye alizaa naye watoto wawili kabla ya kuachana na baada ya kubainika kwamba alichepuka na mrembo Hamisa Mobetto na kumtia mimba, jambo ambalo lilimkera Zari akabeba mabegi yake na kuaga Madale.

Lakini 2019 Diamond aliingia kwenye mahusiano na mwanamitindo wa Kenya na mwanamuziki Tanasha Donna, ambaye alizaa naye mtoto mmoja wa kiume, mnamo Oktoba 2019. Wawili hao waliachana miezi michache baada ya mrembo huyo kujifungua, Tanasha akasepa kwao Kenya.

Makampuni anayofanya nayo kazi

Mnamo 23 Januari 2019, Diamond Platnumz alitambulishwa rasmi kama Balozi wa Pepsi wa Afrika Mashariki.

Mnamo 13 Septemba 2019, Diamond Platnumz alikua Balozi wa Bidhaa ya Parimatch Africa.

Mnamo tarehe 25 Septemba 2019, Diamond alitajwa kama Balozi wa Nice One Brand.

Mnamo Machi 4, 2020, Diamond Platnumz alizinduliwa kama Balozi mpya wa Bidhaa za Coral Paints (Tanzania).

Nyimbo ya Diamond iliyovunja rekodi

Diamond Platnumz miezi 8 iliyopita aliachia ngoma iitwayo waaaah na kuweza kupokelewa kwa mikono miwili na washabiki pamoja na wapenzi wa mziki hasa wapenzi wa muziki wa bongo fleva.

Nyimbo hii iliweza kuweka rekodi kubwa ambayo haikuwahi kuwekwa wala kuvunjwa na msanii yeyeto hapa nchini Tanzania, mashariki na kati. Inasemekana kwamba nyimbo hii iliweza kupata watazamaji milioni 1 ndani ya masaa 8 tu.

Lakini nyimbo hii pamoja na muda mrefu uliopita tangu imeachiwa imeweza kuzidi kutazamwa sana duniani ambapo kwa huu mwezi wa 8 imefikisha jumla ya watazamaji milioni 80. Hii inaonesha dhahiri kwamba Mondi ni msanii mkubwa na anafuatiliwa sana kuliko wasanii wote nchini Tanzania.

Lakini licha ya kuweka rekodi hiyo juzi kati pia nyimbo yake aina ya amapiano imeweza kupata watazamaji jumla ya milioni 1 kwa muda wa masaa kumi na tatu tu. Hivyo kizuri ni kizuri tu lazima kimurikwe na kutazamwa sana. Hayo ni machache tu kuhusu Mondi.