Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 06 27Article 544444

Maoni of Sunday, 27 June 2021

Columnist: www.habarileo.co.tz

Tuitikie Bunge kushiriki katika kutoa maoni marekebisho ya Sheria

Tuitikie Bunge kushiriki katika kutoa maoni marekebisho ya Sheria Tuitikie Bunge kushiriki katika kutoa maoni marekebisho ya Sheria

KATIKA gazeti letu la jana tuliandika kwamba Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imepanga kuanza kupokea toka jana maoni ya wadau kuhusu muswada wa sheria wa marekebisho wenye jumla ya sheria 14 mbalimbali.

Katika taarifa hiyo tuliambiwa pia muswada huo wa marekebisho namba 3 wa mwaka 2021 unafanyiwa kazi kwa mujibu wa kanuni ya 97 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Juni 2020.

Kifungu hicho kina ruhusu Kamati iliyopelekewa Muswada kutoa matangazo au kumwalika mtu yeyote afike kutoa maoni yake mbele ya Kamati hiyo kwa lengo la kuisaidia katika uchambuzi wa Muswada huo.

Kutokana na umuhimu wa muswada huo wa sheria tunapenda kuwakumbusha watanzania na wote ambaow anaitakia mema nchi hii kuhakikisha leo saa 4 asubuhi wawe wamefika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Dodoma kuchambua na kuangalia miswada hiyo muhimu kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kuanzia katiika kaya hadi taifa.

Pia tunapenda kuwashauri wale ambao hawataweza kufika Dodoma kuhakikisha wanatoa mchango wao kwa njia ya posta au barua pepe [email protected] na [email protected] bunge.go.tza ili kuhakikisha kwamba marekebisho hayo yanakidhi haja ya sasa ya maendeleo ya taifa.

Ikumbukwe kwamba ndani ya sheria hizo 14 zinazofanyiwa marekebisho ipo Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sheria ya Mashauri ya Serikali na Sheria ya Bima.

Pia Sheria ya Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya, Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sheria ya Serikali za Mitaa Mamlaka za Miji na Sheria ya Mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili za nchi.

Kiukweli kama ukisoma jedwali la marekebisho ya sheria utabaini kwamba marekebishio yote yaliyokusudiwa na serikali yanagusa wanafamilia na taifa kutikana na umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku, katika uzalishaji mali na umiliki wake.

Suala hili la ushiriki katika kutoa maoni si la kuwaachia wanasheria pekee bali pia watu wengine ambao wanajua kabisa kwamba mustakabali wa maisha yao na ya wengine yamo katika sheria zinazotungwa kuwezesha uwekezaji, uzalishaji na usafirishaji na hata udhibiti wa bidhaa na huduma mbalimbali.

Na hili kwa watu wa kawaida wanaliona hata katika marekebisho yaliyolengwa kuongeza kifungu kwa Tume ya Ushindani kuhusiana na matumizi mabaya ya nguvu ya soko na uunganishwaji na utwaaji wa makampuni.

Tunaamini kwamba Watanzania kwa ajili ya maslahi mapana zaidi ya taifa na wao wenyewe wataitikia wito wa Bunge wa kwenda kutoa maoni yao kuhusiana na marekebisho hayo ya serikali ili kuona kwamba yanaitikia mahitaji halisi ya nchi na wananchi katika kujenga uchumi wa kati wa juu kwa amani na usalama.

Katika hili tunawakumbusha Watanzania kuona haja ya kushiriki kikamilifu katika utunzi wa sheria na marekebisho yake kwa ajili ya ustawi wa nchi na kupata Sheria ambazo zinaangalia uhalisia ili ziweze kutusaidia katika ujenzi wa uchumi unaoambatana na usalama wa watu na mali au huduma zinazozalishwa.