Uko hapa: NyumbaniWallMaoniArticles2021 02 20Article 525580

Maoni of Saturday, 20 February 2021

Columnist: Mwanaspoti

UCHAMBUZI: Simba iwadhibiti Al Ahly maeneo haya

UCHAMBUZI: Simba iwadhibiti Al Ahly maeneo haya UCHAMBUZI: Simba iwadhibiti Al Ahly maeneo haya

 MSIMU wa Ligi ya Mabingwa Afrika uko kwenye harakati zake na wawakilishi wetu Simba wanajindaa na mechi dhidi ya Al Ahly itakayochezwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dares Salaam.

Simba wapo katika kundi A ambalo mbali na Al Ahly kuna pia timu za AS Vita Club ya DR Congo na El Merreikh ya Sudan.

AS Vita na El Merreikh kama ilivyo kwa Al Ahly ni timu kubwa na ngumu zenye historia kubwa ya soka Afrika zikiwa zimewahi kufanya vizuri hapo nyuma.

Tukija katika mchezo ambao Simba watacheza na Al Ahly, wawakilishi wetu hapana shaka watakuwa na mchezo mgumu na wanapaswa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

Kuna sifa za nje na ndani ya uwwnja ambazo Al Ahly wanazo zinazofanya mechi yao dhidi ya Simba hapa iwe ya aina yake.

Kwanza nje ya kiwanja, Al Ahly ni timu kubwa. Unaposema next level wao wako huko kwa maana kwamba wana uwekezaji mkubwa na wako imara kiuchumi. Lakini la pili ni mabingwa watetezi.

Join our Newsletter