Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 12 18Article 579496

Maoni of Saturday, 18 December 2021

Columnist: www.tanzaniaweb.com

Ujio wa Denis Nkane Yanga na mabadiliko ya Namba

Denis Nkane Denis Nkane

Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kinda Mtanzania, Denis Nkane (18) mtoto wa maajabu ( WONDER KID) anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji wa pembeni kwenye Klabu ya Biashara United.

Endapo Yanga wakikamilisha usajili wa kinda huyo, itakuwa imelamba dume na ni msaada mkubwa kwa timu yao pamoja na Taifa kwa ujumla kwakua kijana atakulia katika mazingira mazuri ya kimpira kuliko ilivyo sasa.

Ujio wa Nkane ndani ya Yanga utaleta mabadiliko ya lazima ya namba kwenye nafasi za viungo washambuliaji wa pembeni kwa zaidi ya asilimia 90. Hii ni kutokana na sifa zake alizonazo na majukumu anayosajiliwa nayo.

Nkane ana uwezo mkubwa kukimbia kwa kasi ya juu bila mpira na akiwa na mpira huku umiliki ukiendelea kuwa wake.

Viungo Washambuliaji wa pembeni waliopo sasa wakikimbia kwa kasi ya juu muda mwingi hupoteza umakini na mpira na kupoteza umiliki hatimae kuua shambulizi kusudiwa.

Nkane ni mbishi kwenye ukabaji na ana akili kubwa ya mpira ikiwemo uwezo wake wa kujiweka sehemu sahihi kwa wakati sahihi.

Ana umiliki na kuchezea mpira vizuri (baller) na pasi zake aidha krosi au pasi fupi za kawaida hufika kwa mkusudiwa kwa usahihi wa hali ya juu sana.

Pamoja na uwezo wake, pia uzawa unakingiwa kifua na Kanuni za TFF kuhusu ukomo wa wachezaji wageni itambeba kuingia kikosini. Yanga itaona ni bora kumtumia yeye kuliko mgeni ili nafasi ya mgeni ichukuliwe na mchezaji wa kigeni mwengine kwenye nafasi nyingine inayolazimu.

Mungu ambariki yaliyo bora na kumuepusha na majeruhi yasiyoisha kijana huyu kwenye majukumu yake mapya anayoyaendea kwenye Klabu yake mpya.