Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 09 27Article 559915

Maoni of Monday, 27 September 2021

Columnist: global publishers

Ukweli kuhusu Pauline Zongo

Msanii wa Bongo Fleva Pauline Zongo play videoMsanii wa Bongo Fleva Pauline Zongo

Namfahamu Pauline Zongo tangu enzi za East Coast Team akiwa kama First Lady wa kundi hilo akiwa na wasanii wengine kama AY, Crazy GK, mwana Fa, Abbas, Snare na wengine mwishoni mwa mwaka 1999 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Namfahamu Pauline kwamba chanzo cha hali yake kuwa hivyo si madawa ya kulevya kama watu wanavyosema.

Mwezi mmoja uliopita, Pauline alifanya mahojiano maalum na Global TV na alieleza kiundani alipata ajali mbaya sana ya gari.

Kwenye ajali hiyo, Pauline alikuwa na mwenzake ndani ya gari na yeye akiwa ni dereva, mwenzake alifariki papohapo na yeye alijeruhiwa vibaya sana kiasi kwamba hakuna aliyewaza kama atapona.

Pauline amefanyiwa upasuaji na kuwekwa chuma kwenye miguu yake yote na pia amefanyiwa upasuaji wa kupunguza utumbo baada ya vipandepande vya vioo vya gari kubaki mwilini mwake na kusababisha kuharibika kwa utumbo.