Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 07 08Article 545986

Maoni of Thursday, 8 July 2021

Columnist: eatv.tv

Umemsikia kocha Gomez baada ya kuifunga KMC?

Umemsikia kocha Gomez baada ya kuifunga KMC? Umemsikia kocha Gomez baada ya kuifunga KMC?

Kocha mkuu wa kikosi wa wekundu wa msimbazi Simba, Didier Gomez Da Rosa amewamwagia sifa wachezaji wake kwa kusema walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu jambo lililopelekea kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC usiku wa jana kwenye dimba la Mkapa usiku wa jana.

Submitted by George David on Alhamisi , 8th Jul , 2021 Kocha wa Simba, Didier Gomez.

Mabao ya Simba yamefungwa na Chris Mugalu dakika ya 2' na 44' na kumfanya afikishe jumla ya mabao 12 kwenye msimu wake wa kwanza VPL, mabao 2 nyuma ya vinara wa mabao mshambuliaji mwenzake John Rafael Bocco na Prince Dube wa Azam.

Baada ya mchezo huo Gomez amesema “Tulijua kabisa KMC ni timu nzuri na ina kocha mzuri sana pamoja na kucheza soka safi. Lakini tulicheza kwa nidhamu sana, tulianza mchezo vizuri sana na kuonesha kuutaka mchezo huku tukiwa na lengo la 'ku-wapress' kwasababu wanakawaida ya kucheza kuanzia nyuma”.

Baada ya kusema hayo, Gomez akajinasibu kuwa wao ni mabingwa waliostahili baada ya kufanya kazi nzuri.

“Sisi ni mabingwa, tulistahili haikuwa rahisi na tunajivunia sana”.

Simba ipo kileleni mwa VPL ikiwa imecheza michezo 31, michezo 3 kumaliza ligi huku wakiwa na alama 76 wakiwa wamefunga mabao 71 na kufungwa mabao 13 pekee ilhali Yanga imecheza michezo 32, miwili imesalia kumaliza ligi wakiwa na alama 70, mabao 50 ya kufunga na 21 ya kufungwa.

Utofauti wa mabao ya kufungwa na kufunga ya Simba ni 58 ilhali Yanga ni 29, Ili Yanga imzuie Simba asiwe bingwa basi inahitajika Yanga ishinde miwili miwili ipate alama 6 na kufunga mabao 30 ifikishe alama 76 na kumpiku Simba kwenye mabao huku Simba afungwe michezo yote mitatu iliyosalia.

Kwa upande mwingine, kocha msaidizi wa KMC, Habib Kondo amefunguka na kusema sababu iliyopelekea kufungwa ni kufeli kwenye mpango wa kimchezo na kuwaruhusu Simba kuwa bora.

“Tumefeli kwenye game plan, tumefeli timu nzima na tumefeli kila kitu. Tulipaswa kuadhibiwa katika mchezo huu ukizingatia pia hatukutengeneza nafasi hata moja ndo maana nasema tumefeli kila kitu. Tumefeli kwenye ulinzi, viungo na ushambuliaji, na sisi walimu tumefeli”.

KMC imesalia kwenye nafasi ya 6 wakiwa wamecheza michezo 32 wakiwa na alama 42.