Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 10 03Article 561064

Maoni of Sunday, 3 October 2021

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz

Utakuwa msimu mtamu zaidi wa Ligi Kuu Bar

Utakuwa msimu mtamu zaidi wa Ligi Kuu Bar Utakuwa msimu mtamu zaidi wa Ligi Kuu Bar

MSIMU wa soka wa Ligi Kuu Bara 2021/2022 umeshuhudiwa ukianza, huku wadau wengi wa soka wa ndani na nje ya nchi wakiwa na matumani kibao ya kuona viwango vya ushindani vikiongezeka tofauti na misimu iliyopita.

Matumaini hayo ya mashabiki wa soka yanatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha uwekezaji fedha kwenye haki za matangazo ya runinga kuanzia msimu huu, ambapo kampuni ya Azam Media imewekeza kiasi cha zaidi ya Sh265 bilioni kwa miaka kumi, huku mkataba huo ukianzia msimu huu ambao mechi zake za kwanza zilichezwa wiki iliyopita.

Ukiachilia mbali uwekezaji huo, pia hata idadi ya timu kutoka 20 misimu miwili iliyopita hadi kubakia 16 tu ambazo ndizo ilikuwa lengo la Bodi ya Ligi.

Hilo ni mingoni mwa mambo pia yanayochangia kuongeza kiwango cha ushindani - kwa maana ya kutimiza idadi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu kuwa 16, hivyo kuwepo na urahisi kuanzia katika eneo la uendeshaji na hasa katika eneo la gharama za uendeshaji kwa klabu linaloendana na ratiba ya msimu mzima inayoendana na ukubwa wa kijiografia wa nchi. Katika mechi za ufunguzi tumeshuhudia matokeo mbalimbali ambapo, kwa mfano, timu zilizofanikiwa kupata ushindi mkubwa na kufunga mabao mengi zilikuwa mbili tu - Namungo na Polisi Tanzania ambapo Namungo iliifunga Geita Gold mabao 2-0, huku Polisi Tanzania ikipata ushindi kama huo dhidi ya KMC.

Pia timu nyingine zilizopata ushindi ni za Mbeya City iliyoifunga Prisons 1-0 , Mbeya Kwanza ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji FC wakipata ushindi kama huo dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga wakishinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, huku sare zikipatikana katika mechi mbili tu - Coastal Union dhidi ya Azam FC iliyomalizika kwa kufungana 1-1 na Biashara United dhidi ya Simba iliyomalizika kwa suluhu.

Hivyo ukiangalia matokeo ya mechi hizo za mzunguko wa kwanza kwa jicho la uchambuzi utagundua kuwa timu nyingi kama si zote ziliingia katika mzunguko wa kwanza kwa mikakati ya uchezji inayofanana, yaani hata ngeni zilizopanda daraja na kushiriki msimu huu kama vile Mbeya Kwanza ambayo ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar iliingia na mpango mkakati wa kushinda tu, licha ya kushindana na timu ya Mtibwa ambayo ni moja kati ya zenye uzoefu mkubwa katika Ligi Kuu hata za kimataifa.

Pia hata Geita Gold ambayo ilipoteza dhidi ya Namungo nayo iliingia ikiwa na mpango wa kupata ushindi tu licha ya ugeni wa kushiriki ligi, lakini ilijiweka katika mazingira ya kuwa na ushindani ulio sawa na Namungo, ndio maana iliingia pia na mpango mkakati wa kutaka ushindi ingawa ilishindwa.

Hivyo, hii ilileta picha tofauti na iliyopo katika ligi kubwa duniani kote ambako huwa zinakuwa na mgwanyiko wa makundi matatu kwa timu zinazoshiriki ambayo hata hapa kwetu kwa miaka mingi tumekuwa tukiyaona, ingawa sio makundi rasmi, lakini hujionyesha kwenye msimamo hasa kuanzia mechi za mzunguko wa pili.

Mara nyingi kuna kundi la kwanza ambalo lina timu chache sana, ambapo huwa katika nafasi ya kugombania ubingwa. Kundi hilo kwenye ligi kwa miaka mingi tumezoea kuwa na timu za Simba, Yanga na Azam tu ndizo zinaonekana, huku kundi la pili likiwa na timu zinazopambana kukwepa kuteremnka daraja, ambapo kwa msimu uliopita tulishuhudia zaidi ya timu kumi, ilhali kundi la tatu ambalo pia huwa na timu chache huwa la zile ambazo hazina nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini pia hazina nafasi ya kuteremka darajan hivyo kutokuwa na presha yoyote katika mechi za kumalizia msimu.

Lakini makundi hayo matatu kwa msimu huu yanaonekana kuvutana kutokana na sababu kuu mbili - kwanza ni kila timu kuonekana kujipanga na kuwa na utashi wa kutaka kushiriki mashindano ya kimataifa, hivyo kuongeza ushindani katika nafasi za juu ambapo msimu uliopita ulishuhudia Biashara United ikipata nafasi ya kushiriki michuano ya Shirikisho barani Afrika baada ya kumaliza ikiwa katika nafasi ya nne ya msimamo.

Lakini, sababu ya pili ni ile ya uwekezaji ambapo kuanzia msimu huu kila nafasi itakuwa na thamani tofauti na nafasi nyingine kwa kupata kiasi cha fedha tofautitofauti, yaani timu itakayomaliza katika nafasi ya 12 haitapata fedha sawa na itakayomaliza ikiwa nafasi ya sita. Vilevile ile ya nafasi ya sita haitapata fedha sawa na timu iliyopo katika nafasi ya tano.

Ni kutokana na mazingira hayo ndio maana tunaona timu za KMC, Namungo, Polisi Tanzania, Dodoma Jiji na Mtibwa zikijipapatua kwa vitendo kuwa na lengo la kutaka nafasi za juu - yaani kupambana na Simba, Yanga pamoja na Azam na kuonekana kuwekeza katika maeneo yote kuanzia kwenye wachezaji hadi katika mabenchi ya ufundi.