Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 06 08Article 541648

xxxxxxxxxxx of Tuesday, 8 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Utashi wa kisiasa wasaidia wanawake kuwania uongozi

NAIBU Spika, Dk Tulia Ackson amesema utashi wa kisiasa hapa nchini umekuwa chachu ya wanawake kushika nafasi za uongozi.

Dk Tulia aliyasema hayo wakati wa kufungua kongamano la siku moja la wanawake wabunge liloandaliwa na Kituo cha Usuluhishi (CRC) kwa kushikikiana na Shirika la kihabari (FEMnet) ikiwa ni kutekeleza kutekeleza Mradi wa Wanawake na Uongozi katika siasa.

Alisema utashi wa kisasa hapa nchini umekuwa chachu ya kuongezeka na kutoa fursa kwa wanawake kushiriki kwenye uongozi.

“Ni sawa watu tunafurahia tuna Rais wa kwanza mwanamke hapa Tanzania, ni uhalisia hiyo nafasi imepatikana kutokana na utashi wa kisisa uliopo nchini. Mama (Rais Samia Suluhu Hassan) alionesha uwezo wa kwamba anaweza kuwa Makamu wa Rais na palipotokea nafasi ya makamu wa rais kuwa rais akapata fursa hiyo.”

Dk Tulia alisema kitakwimu, Tanzania imepiga hatua kwa wanawake kuwa kwenye uongozi na kuwa Rais Samia amefanya kazi nzuri ya kuongeza idadi ya wanawake kwenye nafasi ya uongozi.

“Tukiangalia uteuzi wa hivi karibuni alipoteua makatibu tawala wa mikoa wanawake ni asilimia 46, hii inaonesha tunaendelea kupanda. Kwa upande wa mawaziri na manaibu waziri wako 11 kati ya 51, sasa ukichukua na wanawake waliopo bungeni unaweza kuona asilimia iko chini lakini ukiangalia kwa uwiano ni dhahiri tunapiga hatua,”alisema.

Naye mwakilishi wa FemnetProg, Doroth Otieno alisema kazi ya taasisi hiyo ni kuongeza idadi ya wanawake katika kushiriki katika siasa.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Rose Reuben alisema vyombo vya habari vina jukumu la kubeba na kuinua wanawake katika suala zima la uongozi.

Join our Newsletter