Uko hapa: NyumbaniWallMaoniArticles2019 11 15Article 487915

Maoni of Friday, 15 November 2019

Columnist: mwananchi.co.tz

Vitu vya kukagua kwenye gari kila siku kabla ya kulitumia

Vitu vya kukagua kwenye gari kila siku kabla ya kulitumia

Unapotaka kutumia gari kwa safari yoyote ile, hakikisha kuwa gari liko salama ili uweze kufika salama. Kuna vitu vichache vya kawaida ambavyo unatakiwa kuvi-kagua kila asubuhi kabla ya safari.

Haijalishi gari lako lilikuwa kwe-nye hali gani wakati umelifikisha na kuliegesha. Vitu hivyo ni hivi vifuatavyo:

Kiasi cha upepo katika tairi

Kila aina ya tairi huwa na kiwan-go fulani cha upepo unaotakiwa kuwa nalo. Ni vyema kuangalia kiwango cha upepo kama kipo cha kutosha au la! ikiwa kipo chini ya kiwango unapaswa uongeze.

Kuendesha gari ambalo tairi lina upepo mdogo ni hatari sana kwani uwezekano wa gari lako kuyum-ba na kutoka nje ya barabara ni mkubwa sana jambo ambalo lin-aweza kusababisha ajali, pia tairi likiwa na upepo mdogo italaz-imu gari kutumia mafuta mengi ili liweze kwenda kasi tofauti na matairi ambayo yana upepo katika kiwango kinachotakiwa.

Kagua taa zote kuanzia taa za mbele, taa za kuegesha gari, taa za ukungu, taa za ishara, taa za breki, taa za kwenye namba ya gari. Taa zote zinatakiwa ziwe zinafanya kazi hata kama ni mchana maana zipo zinazotumika muda wote.

Ni muhimu kuhakikisha taa hizi zinafanya kazi ili kurahisisha mawasiliano unapokuwa baraba-rani, kwa mfano ukitaka kuingia upande kushoto/kulia utatakiwa kutoa ishara. Ni kosa kisheria endapo utaka-matwa unaendesha gari ambalo taa zake hazifanyi kazi kwani unaweza kusababisha ajali kwa watumiaji wengine wa baraba-rani.

Maji ya wiper

Kabla hujawasha gari kabla ya kuanza safari, unashauriwa kukagua maji ya wiper ili kuhakik-isha yapo ya kutosha. Maji haya hutumika kusafisha kioo cha mbele cha gari lako au nyuma (kwa baadhi ya magari) endapo kitachafuliwa kwa namna yoyote. Je, utakuwa katika hali gani enda-po umerushiwa maji machafu kwenye kioo halafu kwenye gari lako hauna maji ya wiper?.

Endapo utawasha wiper za gari ili kusafisha kioo cha mbele, hazi-tosafisha na badala yake zitazidi kuusambaza uchafu na kufanya ushindwe kuona vizuri baraba-rani. Hapo hutoweza kuona mbele na kutokana na mshtuko mkub-wa utakaokuwa nao wakati huo, uwezo wa kulitawala gari lako utakuwa ni mdogo na hivyo kusa-babisha ajali.

Kilainishi cha injini (engine oil)

Umuhimu wa kukagua kila mara ni kuweza kujua kiasi kilichopo na ubora wake kama imefika wakati kubadilishwa au la.

Matumizi makubwa ya kilaini-shi hiki ni kuzuia vyuma ndani ya njini kusagana kutokana na msug-uano wakati gari likifanyakazi na pia inaisaidia injini kufanya kazi kwa urahisi zaidi.

Coolant

Coolant ni kimiminika ambacho hutumika katika kupooza injini ya gari linapokuwa linatumika.

Kutokana na gharama kubwa ya vimiminika hivi, watu wengi wak-ishavinunua huchanganya na maji na kisha kuviweka katika rejeta ya gari, lakini kiusahihi vimimika hivi vinatakiwa kuwekwa kwenye rejeta bila kuchanganywa na maji.

Unashauriwa kuweka COOLANT kwenye rejeta bila kuchanganya na maji kwa sababu itakaa muda mrefu tofauti na unapochanganya na maji ambapo gari litachemsha lakini kumbuka kuwa kiwango cha maji kuchemka (boiling point) ni kidogo ukilinganisha na ‘coolant’.

Maji yanapochemka huwa mvuke na hivyo itakulazimu kila mara kuongeza maji katika rejeta.Faida nyingine ya kutumia coolant badala ya maji ni kuwa, yenyewe husaidia kuzuia rejeta ya gari isi-pate kutu, hivyo unapoweka maji, unaharibu rejeta kwani itashika kutu.