Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 09 29Article 560413

Maoni of Wednesday, 29 September 2021

Columnist: www.habarileo.co.tz

Waandishi habari walivyo chambo kwa Covid-19

Waandishi habari walivyo chambo kwa Covid-19 Waandishi habari walivyo chambo kwa Covid-19

"Chanjo suluhisho la usalama wao"

KUNDI la waandishi wa habari ni miongoni mwa makundi ambayo yako hatarini kupata maambukizi yavirusivya corona hii ni kutokana na shughuli zao za kila siku kuwa na mwingiliano.

Tahadhari muhimu za kiafya zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na kuepuka mikusanyiko kwa kuweka nafasi kati ya mtu na mtu,kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono.

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za Julai 8, mwaka huu watu 408 walikuwa wamepata maambukizi ya wimbi jipya la Delta huku watu 284 wakipumulia mashine za oksijeni.

Wizara imeendelea kusisitiza watu kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo kwa kutoa mwongozo ambao unataka watu kunawa mikono kwa maji tiririka na kujitakasa mikono.

Miongozo mingine ni kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima sehemu mbalimbali ikiwemo kupunguza idadi ya abiria katika vyombo vya usafiri (level seat).

Kuvaa barakoa sehemu za mikusanyiko kama sokoni, hospitalini, taasisi za kiserikali na binafsi, vyombo vya usafiri na mikusanyiko mingine.

Lakini Je ni waandishi wangapi wanazingatia tahadhari hizo?

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mwanza Press Club, Edwin Soko asilimia 75 ya waandishi waliopatiwa mafunzo kwa njia mbalimbali wanafata maelekezo ya kujikinga na ugonjwa wa Covid -19.

“Kuna asilimia 25 iliyobaki hawa hawafati tahadhari huenda ni kwasababu hawajafikiwa au kupuuza,”anasema Soko.

Jitihada zinazofanywa zinaweza kuwa msaada mkubwa kwa waandishi wa habari kupata uelewa na kuwaelimisha jamii.

Soko anabainisha kuwa kupitia club yao wanaandaa mikutano na midahalo kuhusu Covid-19 na chanjo.

“Katika mikutano hiyo kuna vitu tunakubaliana kama miongozo itakayosaidia waaandishi kufanyakazi zao na kujikinga ,Moja ni kuweka distance kati yake na chanzo cha habari, pili kuwa makini na kutoshirikiana vifaa.

“Tunawafundisha jinsi wanavyotakiwa kufanyakazi na namna ya kuvaa barakoa na kubadilia,”anafafanua.

Aidha wanafanya uandaajiwa mikutano ya kimataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ilikukutanisha wataalamu wa afya mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu.

“Wataalamu wanawaeleza ili kumfanya mwandishi kuwa na weledi na kuweza kuchuja taarifa sahihi.

KWANINI WAANDISHI HAWAZINGATII TAHADHARI?

Mwandishi wa habari za afya, Harieth Makweta anasema bado hakuna mkazo wa waandishi kuchukua tahadhari za kujingana Covid -19 licha ya kuwa wanaandika habari hizo.

Makweta anaeleza kuwa waandishi wa Habari wanaochukua tahadhari ni wachache na hii ni kutokana na kupuuzia tahadhari.

“Tunaona wengi wanaenda kucover story hawaja vaa barakoa na wengine hawa na sanitizer lakini wanaripoti habari za covid wao hawachukui tahadhari za aina yoyote ile.

Anaongeza “Licha ya kwamba wanapewa elimu lakini bado jitihada za tahadhari hamna na tunadhani kwamba tunaweza kuwapatia watu wengine elimu na sisi hatuzingatii.

Anasema kuwa mwamko bado ni mdogo na wanapaswa kukumbushwa wao wenyewe kuchukua tahadhari.

James Salvatory ni Mwandishiwa Times Fm anasema kwa kiasi kikubwa bado waandishi hawazingatii tahadhari na hii ni kutokana na mtazamo wa uongozi uliopita.

“Na hii ni kwa wananchi pia wapo wanaoamini kuwa hakuna corona licha ya serikali kuendelea kusisitiza kuwa watu wa chukue tahadhari,”anaeleza.

TUNAFANYA JITIHADA HIZI

Kundi la Habari ndio wanaotegemewa kufikisha elimu kwa jamii hasa kuhusu janga la Covid 19.

Taasisi zinazohusika na masuala ya kihabari zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha waandishi wanapata elimu ya namna ya kujikinga.

Miongoni Mwa taasisi ambazo zinajihusisha moja kwa moja kuhakikisha waandishi wanapata uelewa ni Taasisi ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TAN).

Kaimu Mkurugenzi wa MISA TAN Andrew Marawiti anasema jitihada kubwa wanayofanya kuhakikisha waandishi wanajikinga na virusi vya Covid 19 nikutoa elimu kwa njia ya mafunzo wanayoandaa.

“Tunatoa mafunzo kwa waandishi na bado tunaendelea kutoa,hivi karibuni mwezi wa saba tulifanya semina ya kuwajengea uelewa waandishi kuhusu namna ya kujikinga na pia kuandika habari za corona.

“Na pia tuna mpango wa kuwa na mafunzo zaidi na tuko kwenye mazungumzo na wadhamini wawili na mmoja tuko katika hatua ya maandiko ,lakini pia tunaonesha mifano wakati wa mafunzo tunafata tahadhari zote za kifya,”anabainisha Marawiti.

Anashauri kuwa ni vyema waandishi wakazingatia hatua za kujikinga pindi wanapokuwa katika majukumu yao.

“Bado elimu inahitajika sio kwa waandishi tu hata kwa wananchi walioko pembezoni hivyo waandishi wa habari wanatakiwa kuwa mfano kwa jamii,”anaeleza.

HabariLEO pia ilizungumza na Mkurugenzi wa Baraza la Habari Tanzania(MCT),Kajubi Mukangaja,anasema mara baada ya kutokea mlipuko wa virusi vya corona baraza hilo liliandaa mwongozo wa kuripoti kwa weledi na usalama.

Mwangozo huo ambao ulisambazwa kwa waandishi wa habari kupitia njia mbalimbali pia unapatatikana katika tovuti ya MCT.

Kajubi anasema jitihada zingine walizofanya ni kuwasiliana na wahariri wa vyombo vya Habari ili kuhakikisha wanawasaidia waandishi wao kujikinga wanapokuwa kazini.

“Sisi tunatoa mifano ya kujikinga kwa kuweka barakoa na vitakasa mikono getini ,hatufanyi mikutano wala semina kwa kukutana kila kitu tunafanyia mtandaoni kwasababu ya kujikinga.

“Hata hafla ya utoaji tuzo za EJAT ni wachache tu walihudhuria wengine walifatilia kupitia mtandaoni kwa link maalum hivyo tunazingatia afya za waandishi,”anafafanua Kajubi.

Chama cha waandishiwa Habari Wanawake (TAMWA) pia wameeleza namna wanavyosaidia waandishi wa habari kujinga na virusi vya corona.

Mkurugenziwa TAMWA, Rose Ruben ,anaeleza kuwa taasisi hiyo inafanya jitihada nyingi tangu kuanza kwa ugonjwa huo mmoja ikiwa ni kuzungumza na wamiliki wa vyombo vya Habari.

“Tumezungumza nao kuwapa vitendea kazi waandishi wanapokuwa katika majukumu yao ikiwemo barakoa na sanitizer.

Anasema jitihada nyingine ni kuhakikisha waandishi wanapewa kipaumbele katika kupata chanjo ya Covid 19.

“Lakini pia tunawaelimisha kuwa baada ya kupata chanjo ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya kwani mwandishi wa habari anaenda popote,”anabainisha.

Irene Mark ni Mwenyekiti wa Clabu ya waandishi Mkoa wa Dar es Salaam( DCPC) anabainisha kuwa utoaji wa mafunzo ya mara kwa mara unaongeza jitihada za waandishiwa Habari kujikinga.

Anasema DCPC kwa kushirikiana na Muungano wa clabu za Habari Tanzania(UTPC) wana fomu maalum inayojazwa ambayo inaeleza kama mwandishi amepashida.

“Kupitia hiyo fomu tunaagalia kama ni shida ya haraka tunawasiliana na chama cha vilabu Tanzania (UTPC) ,baraza la Habari na LHRC kuona namna gani tunawasaidia.

“Lakini pia tunawafundisha waandishi kuwa afya zao ni muhimu kuliko kitu chochote na akiweza kulinda afya ataweza kufanyakazi,”anaeleza.

Anasema kwa kipindi cha mwaka jana waliweza kugawa vifaa mbalimbali vya kujikinga.

“Kila mwanachama alipata vifaa kama barakoa na vitakasa mikono (sanitizer).

Hata hivyo anasema kwasasa asilimia kubwa ya waandishi hawachukui tahadhari licha ya jitihada hizo.

“Wengine ni kwasababu ya chanjo na sio wengi wanaozingatia ni wachache mno,”anasema.

Saed Kubenea ni Miongoni mwa wamiliki wa chombo cha Habari hapa nchini anasema jitihada wanazofanya ni kuwasisitiza waandishi wao kujikinga wanapokuwa kazini.

“Kuhusu kujikinga ni suala la mtu binafsi kama hana mwamko haiwezi kusaidia na pia kwenye media zetu kipindi hiki kumekuwa na mtikisiko wa uchumi hivyo kuwapa vifaa mara kwa mara inakuwa changamoto.

“Nawashauri waandishi wenyewe kwanza wajijali na kuchukua tahadhari wanapokuwa kazi,”anasisitiza.

MOAT TUNAANGALI HILI

Wamiliki wa vyombo vya habari wananafasi kubwa kuhakikisha kuwa waandishi wanapata vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona.

Inagawa ni miongoni mwa majukumu yao lakini Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) Samwel Nyalla anasema hawawezi kulazimisha hilo badala yake wanajikita zaidi katika sera na biashara.

“Hatufanyi kazi kwa command na hatuingii ndani kwa wawekezaji wako wa aina mbalimbali hivyo sisi tunafanyakazi na wenye vyombo na sio waandishi wa habari lakini ni muhimu kila mwandishi kujali afya yake anapokuwa kazini,”anasema Nyalla.

MAMBO YA KUZINGATIA

Soko anasema Kundi la waandishi lipo katika hatari na linatakiwa kuchua hatua katika kujikinga.

“Kazi za waandishi ni kuhabarisha na kuelimisha kuhusu covid hivyo waendelee kuwaelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo pamoja na kuzingatia kujikinga,”anaeleza.

Mark anawasisitiza waandishi wa habari kuwa hakuna habari bora zaidi ya maisha yao.

“Ukitoka kwenye uandishi wa habari ujue wewe ni baba ,mama na unandugu usipofata tahadhari utahatarisha maisha yako na hautafikia malengo yako,”anaeleza.

Mkurugeziwa TAMWA Rose Ruben anasema wanaendelea kusisitiza waandishi kuchukua tahadhari.

“Wajilinde wenyewe kwani maisha niyao na pia wanapojilinda wanawalinda na wengine,”anashauri.

CHANJO NI MUHIMU

Agosti 4, Mwaka huu dozi 1,008,400 za chanjo zilikuwa zimesambazwa kwenye mikoa yote 26 na inatolewa kwenye vituo zaidi 550 nchi nzima.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa anasema jumla ya Watanzania zaidi ya 345,000 wameshapatiwa chanjo hiyo na kazi ya utoaji chanjo hizo inaendelea.

Wataalamu wa afya wanasema chanjo ni njia moja wapo ya kujingana maambukizi ya virusivya corona.

Martha Magawa ni miongoni mwa waandishi waliopata chanjo anasema ni muhimu waandishi kupata chanjo kwa hatua zaidi za kujikinga.

“Serikali imewapa kipaumbele kwa waandishi wa Habari kupata chanjo tangu siku ile imezinduliwa na Raisa Samia.

Mjumbe wa baraza la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Nevvile Meena,anasema kundi la waandishi ni muhimu kupata chanjo kwani ni njia moja wapo ya kujikinga.

“Kisanyasi chanjo inapunguza watu kupata ugonjwa mkali ambao utawaumiza na uwezekano wa kufa haimaanishi kuwa hata kufa.

“Na ukizingatia waandishi wa Habari ni sehemu ya jamii hatuwezi kukwepa maambukizi na sisi tupo kwenye hatari,”anaeleza.

Anasema hatari huja pale kazi zao zinapokuwa za kuchangamana na watu kwani inabidi watoke waende sehemu na kwenye mikusanyiko.

“Kwa hali hiyo huwezi kuondoa umuhimu wa waandishi wahabari kuchanja hivyo chanjo ni njia moja wapo ya kuzuia maambukizi,”anasisitiza Meena.

MIKAKATI WA SERIKALI

HabariLEO ilifanya mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Prof Abel Makubi ambaye anasema waandishi ni kundi ambalo linaangaliwa zaidi na serikali katika kujikinga na virusi pamoja na kuelimisha jamii.

“Kwanza kwakutambua umuhimu wa waandishi wa Habari serikali ilitoa kipaumbe ya wao kupata chanjo utakumbuka wakati zoezi linazinduliwa pale ikulu na waandishi waliopo walipata chanjo na hii ni njia moja wapo ya kujikinga.

“Lakini pia serikali imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi kuhusu ugonjwa huo ili na waowaende kuwahabarisha jamii namna ya kujikinga kwani tunawategemea zaidia wao,”anaeleza Prof Makubi.

Anasema anawasihi waandishi kuchukua tahadhari wanapokuwa katika majumu yao na pia kupata chanjo ya Covid -19 kama hatua ya kujikinga.

“Jamii inawategemea na kuwatazama wanatakiwa kuwa mfano mzuri katika kujikinga na kupata chanjo ya corona,”anabainisha.