Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 08 17Article 551980

Maoni of Tuesday, 17 August 2021

Columnist: https://www.ippmedia.com/

‘Wabongo’ kwa hili msihofu tena chanjo ya Johnson

Chanjo ya Jansen Chanjo ya Jansen

TAARIFA za hivi karibuni za utafiti kuhusu chanjo za UVIKO-19 zinaonyesha kuwa wataalamu wameanza kuikubali chanjo ya Johnson & Johnson kuwa ni madhubuti zaidi kukikabili kirusi cha delta.

Taarifa za awali zinasema chanjo hiyo ina uwezo mkubwa dhidi ya aina hiyo ya kirusi katika majaribio yaliyofanyika Afrika Kusini.

Utafiti ulionyesha kuwa J&J ina uwezo kwa asilimia 71 kuzuia kulazwa hospitalini endapo mtu anaambukizwa corona kutoka kirusi delta kinachohofiwa kutokana na kasi yake kubwa ya kuambukiza.

Delta imeamsha upya corona duniani, nchi zikianza kusitasita kutabiri kupiga hatua zaidi kufungua uchumi, kufanya shughuli kawaida.

Licha ya kuwa utafiti huo hausemi kuwa ukiwa umepata chanjo ya aina hiyo hutaambukizwa, bado unaashiria kuwa unakuwa na matumaini ya kuwa salama zaidi kuliko ukiwa umepata chanjo ya aina tofauti.

Hali hiyo ni faraja kwa sehemu kubwa ya wanaofuatia chanjo hapa nchini kwani kwa upande wa Bara ni ya aina hiyo, huku Zanzibar wakiwa wametangulia kutoa chanjo ya Sinovac ya China.

Ile ya China ni mojawapo ya chanjo zinazohitaji kuchanjwa mara mbili, wakati J&J ni mara moja na kuelezwa kuwa ina nguvu ya ziada.

Taarifa zinazofanana za magazeti makubwa ya kila siku kama New York Times, Washington Post na New York Post yote ya Marekani, zinaeleza na kunukuliwa na mitandao ya habari hivi majuzi kuwa jaribio hilo liligusa wafanyakazi wa sekta ya afya karibu 480,000.

Lilikuwa ni jaribio la kwanza ‘lililojikita katika hali halisi’ kuhusu chanjo hiyo ya dozi moja chidi vya maambukizi ya kirusi cha delta.

Taarifa ya New York Times inasema matokeo hayo yanaendana na utafiti wa ndani katika maabara uliochapishwa na kampuni hiyo mwezi uliopita ukioonyesha kuwa chanjo hiyo ya dozi moja inatoa ulinzi bora dhidi ya maambukizi. Ni kwa uwezo wake wa kuzuia kulazwa, endapo unaambukizwa.

Utafiti huo uliopewa jina la Sisonke ulionyesha kuwa J&J ina uwezo hadi asilimia 71 kuzuia maambukizi ya delta na takriban asilimia 96 ya ulinzi dhidi ya kifo.

Utafiti huo ulikuwa bado haujawakilishwa katika majarida makubwa ya utafiti tiba kupitiwa na wataalamu wengine kabla ya kuchapishwa rasmi, hali ambayo haikuzuia kutolewa matokeo ya utafiti huo kama yakinifu, kwani unafuatia uchunguzi kimaabara wa uwezo wa chanjo hiyo katika maeneo yote matatu ya maambukizi na ustahimilivu wa mtu aliyepata chanjo hiyo.

Ni taarifa ambazo kwa muda mfupi zinaweza kubadilisha sura ya uhitaji wa chanjo moja au nyingine, kwani kilichotangulia kuhusu chanjo hizo awali ilikuwa ni athari zinazohofiwa, ambako J&J na AstraZeneca zilikuwa zikiogopwa kwa kugandisha damu.

Kuna utafiti mwingine ambao haujapewa kipaumele kihabari na katika kufanya maamuzi, zisivuruge makubaliano kati ya watengeneza chanjo mataifa tofauti na wahitaji, au mamlaka za nchi zinazoagiza chanjo, mashirika binafsi au kampuni yanayohitaji chanjo kwa matumizi ya ndani kwa wafanyakazi wake zisianze kubadili maamuzi.

Utafiti huo uko makundi mawili au unalenga maeneo mawili muhimu, la kwanza likiwa ni kupima uwezo wa jumla wa kuambukizwa upya baada ya kupata chanjo na hasa kwa kirusi badilika cha delta, na eneo la pili ni tofauti, yaani kutoa dozi moja badala ya mbili.

Kwanza hali hiyo inapunguza usumbufu na uoanishaji wa taarifa za chanjo, na sasa inaelekea kuna manufaa ya ziada.

Kwa haraka, ilikuwa imeanza kuonekana kuwa Sinovac ya China na Sputnik V ya Russia zilikuwa labda ni dhaifu kidogo katika kutoa kinga ya kuambukizwa tena.

Iliyoonekana nzuri zaidi ni Pfizer/BioNTech halafu, ikifuatiwa na J&J na AstraZeneca kutokana na tatizo la kuganda damu kwa baadhi ya waliopata chanjo hizo.

Utafiti huo wa Afrika Kusini umekuja kama jibu kwa taarifa za kitaaluma awali kuwa J&J inaweza isiwe na kinga ya kutosha dhidi ya delta.