Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 08 17Article 552043

Maoni of Tuesday, 17 August 2021

Columnist: Tanzaniaweb

Watoto walivyogeuza tatizo la ngozi kuwa fursa

Watoto walivyogeuza tatizo la ngozi kuwa Fursa Watoto walivyogeuza tatizo la ngozi kuwa Fursa

Wazo la Biashara hukua ndani ya mtu kwa njia mbali mbali, hadithi moja ya mjasiamali inaweza kutofutiana na mwingine.

Kauli hiyo inakuja baada ya Vijana wawili ambao ni ndugu Ismat Rajabali mwenye umri wa miaka 19 na Nawali Rajabali mwenye umri wa miaka 17 kusema walipata wazo lao la biashara kutokana na matatizo ya ngozi. Walitumia dawa nyingi za viwandani kuepuka tatizo hilo haikusaidia zaidi liliwasababishia madhara ya kuwashwa na kutokwa na chunusi.

Ndipo sasa wakajaribu kutumia bidhaa za asili kukabiliana na tatizo hilo. Waliamua kutumia asali na manjano, na huo ndio ukawa mwanzo wakuanzisha kampuni ya Sugarberry ambayo ipo Dar es Salaam, kampuni hiyo imeanzishwa mwaka 2017 wakiwa katika umri mdogo wa miaka 16 na 14.

"Tunatokea katika familia yenye matatizo ya ngozi na hii ilitufanya sisi kutengeneza bidhaa za ngozi za asili" wanasema vijana hao.

"Tulianza kutengeneza bidhaa ndogondogo kama scrub, sabuni, mafuta ya maji, sabuni ya kuogea ya maji na mafuta ya mdomo. Tulitumia malighafi kutoka Supermarket" Amesema Nawal.

Wawili hao wanadai kujifunza zaidi nyumbani licha ya kusomea masomo ya sayansi, na kwa sasa hawasomi tena wameelekeza nguvu zao katika kutengeneza vipodozi vya asili.

Kwa upande wa mahali pakuuzia bidhaa zao, Vijana hawa walianza na mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii yaani Facebook na Instagram kwasababu hawakuwa na uwezo wakumiliki Duka. Walifanyakazi ya ziada kuhakikisha wanapata wateja huko mtandaoni.

Miaka mitatu badae wakafungua Duka maeneo ya Masaki na kariakoo. Tawali anasema walitakiwa kuanza kuwaamanisha wateja kutumia bidhaa zao na kama wangetambulika mapema wakiwa katika umri mdogo wateja wasingechukulia uzito suala la wao kutengeneza bidhaa.

" Ndani ya miaka hii mitatu ya kusimamia kampuni ya Sugarberry na kaka yangu Ismat imetufanya kuthamini na kujua maana halisi ya kuendesha biashara" Alisema Nawal.

Kwa sasa kampuni Sugarberry inazalisha bidhaa 22 baadhi kati ya hizo zinatambulika kwa majina ya Night Violet Body Butter, Rose Geranium Body Oil, Lavender Lilac Body Oil, White Lily Body Lotion, na Botanical Face Oil.

Kampuni ya Vijana hao ambao ni ndugu huagiza malighafi ya kutengenza bidhaa zao kutoka, Kenya, India, Afrika ya Kusini, Ghana na Uingereza.