Uko hapa: NyumbaniUkurasaMaoniArticles2021 09 05Article 555379

Maoni of Sunday, 5 September 2021

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga Day ‘tuvute soksi’ shuguli katika pitch si lelemama!

KWAKO JESSE JOHN: Yanga Day ‘tuvute soksi’ shuguli katika pitch si lelemama! KWAKO JESSE JOHN: Yanga Day ‘tuvute soksi’ shuguli katika pitch si lelemama!

NAWASALIMU mashabiki na wapenzi wa Mwalimu Kashasha na wasomaji wengine wote nawapa pole kwa kuondokewa na gwiji huyo.

Sasa nimeachiwa kijiti cha Mwalimu kwa niaba ya uongozi wa Mwanaspoti. Sintokuwa kama yeye ila nitajaribu kupita katika nyayo zake, kwani alikuwa pacha wangu katika utangazaji na kuna mavitu ameniachia nitashea nanyi.

Nawapa pole sana na nawaahidi kuandika makala jinsi nilivyomfahamu KASHASHA.

Niwapongeze ‘Wananchi’ katika wiki yao walifanya huduma za jamii Bara na visiwani pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji.

Kwa kweli mlitakata katika hili na imekuwa kawaida kwenu. Mchezo wa mpira wa miguu unahusisha kusanyiko la watu ‘social sports gathering’, ingawa kuna wale wasioweza kujumuika hasa kutokana na udhaifu wa kibinadamu, mmewafikia hospitalini, masikini, yatima na wasiojiweza ikiwa ni pamoja na kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki na mlifanya usafi katika malalo yao.

Siku ya tamasha, Agosti 29, mashabiki mliinasibisha na kauli mbiu ya ‘Sisi tuna watu’ licha ya kuwepo kwa kasoro kadhaa katika uratibu wa shughuli yenyewe na hasa katika kushadadiza tamasha. Sio siri utaratibu haukuwa maridhawa hasa washereheshaji na hili lilionekana dhahiri wakati wa utambulisho wa wachezaji.

Wachezaji walipotoka na suti zao wakiwa na bango la mdhamini walionekana kuzagaa katika eneo la kukimbilia, bango la mdhamini halikupewa thamani kuwekewa kibebeo yaani zile fimbo pembeni ili lisijikunjekunje wakati wa kulionyesha, wimbo wa timu pia haukupewa thamani. Ni tunu ya timu kwa wanaojua mfano wimbo ule wa Liverpool ‘You Will Never Walk Alone’, tazama unavyoimbwa na mashabiki wakati wa mbungi, wachezaji wanavyojaa upepo dimbani, spirit ya kufa mtu, sasa unaimbwa na KABWILI? Ni mzaha wa hali ya juu.

Katika burudani hasa ya gwiji Mzee mzima Koffi Olomide, waratibu walichelewesha utamu, aliingia kwa kuchelewa pamoja na kumuita aingie mara kwa mara. Pamoja na hilo, walichemsha kumuimbisha bila kutumia live band. Kama unataka afanye ‘to the maximum’ waratibu wangeandaa live band hapo ndo ‘shoo shoo’ ya Mopao tungeiona, hapo haki haikutendwa na hela zimeenda bure.

Katika utambulisho wa wachezaji nani alipaswa kuanzwa, DJUMA SHABAN au ilipaswa HAJI MANARA atambulishwe kwanza? Alitambulishwa Djuma kwanza halafu zoezi likabadilishwa akatambulishwa HAJI na ndiye aliyeendelea kuwatambulisha wachezaji kwa staili ileile aliyokuwa akiitumia alipokuwa Simba na kwa kweli ilivutia mashabiki, kasoro iliyojitokeza wachezaji kujipanga katika mstari eneo la pitch kisha wakabadili na kurudishwa jukwaani, hii ilitia dosari sana kana kwamba walikuwa wanagombea nani atambulishe.

Tukimalizia katika mchezo wenyewe, kama Yanga wanataka kutwaa makombe, wachezaji licha ya kutokaa pamoja kwa muda na changamoto za kambi kule Morocco, walipaswa kuonyesha thamani yao kwa mashabiki waliowapa heshima kubwa, wachezaji walipaswa kwenda beyond na plan za mwalimu, walipaswa kujiandaa wao wenyewe self-discipline, and self-preparation ili kuweza kumudu tukio la mechi. Lakini walishindwa kwa maana walikata upepo kipindi cha pili na hili ni tatizo la Yanga. ‘Pitch’ sio ya kuweka mduara na kucheza baringobaringo, inapaswa wajipange kisawasawa, kuoneysha level of commitment, fighting spirit na kuwa aggressive katika kupigania ushindi kwa jasho na damu, vinginevyo wana muda kujisahihisha na wasiweke akilini kama wanavyoelezwa kuwa yeyote wa nje afe kwa Mkapa na hasa mnyama... ILI KWENDA PEPONI LAZIMA KABLA YA KUFA UISHI MAISHA YA MFANO sio kelele kelele.